Ahmed Ally "Juma Mgunda Atatuvusha Simba Imani Ma



Uongozi wa Simba SC umesema hautafanya haraka katika suala la kumsaka Kocha Mkuu mpya, licha ya mchakato huo kuwa sehemu ya vikao vya Bodi ya Wakurugenzi.


Simba SC ipo kwenye mpango wa kusaka Kocha Mkuu mpya katika kipindi hiki, baada ya kuachana na Kocha kutoka Serbia Zoran Maki aliyetimkia nchini Misri kwa makubaliano ya kuvunjwa kwa mkataba wake.


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema Uongozi wa juu unaendelea kutafuta Kocha Mkuu mpya kwa utaratibu, huku wakiamini kikosi chao kipo kwenye mikono salama ya Makocha wazawa Juma Mgunda na Seleman Matola.


Simba SC kufuta rekodi mbaya Angola

“Mchakato wa kutafuta kocha unaendelea lakini hatuna presha ya kutafuta kocha kwa haraka kwa sababu Mgunda na Matola wametuaminisha kuwa wanaweza na sisi tumewaamini. Hatuna haraka” amesema Ahmed


Katika hatua nyingine Ahmed Ally amesema Simba SC mwezi huu inakabiliwa na ratiba ngumu kwenye Michuano ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, lakini wanaamini chini ya Kocha Juma Mgunda kikosi chao kitapambana na kufanya vizuri.


Amesema kimtazamo baadhi ya Mashabiki wa Soka la Bongo hawaamini kama Mgunda ataweza kufanya vizuri kwenye mtihani huo mgumu, lakini Uongozi una imani kubwa na Kocha huyo mzawa.


Simba SC kwenda Angola kwa ndege maalum

“Tuna michezo mitatu muhimu mwezi huu, Mgunda anaweza kutupatia ushindi, wapo walianza kumbeza kwa kusema mwezi huu ndio watafahamu uwezo wake kama anabahatisha ama la, lakini kwetu kama Uongozi tunaamini Kocha wetu watafaulu mtihani huu mzito” amesema Ahmed Ally


Oktoba 23 Simba SC itacheza dhidi ya Young Africans, kisha itakutana na Azam FC Oktoba 27 katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara, pia itapapatuana na Mabingwa wa Angola Premeiro De Agosto kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ikianzia ugenini Oktoba 08 na kumalizia nyumbani Dar es salaam Oktoba 16.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad