Watu saba wa Familia moja akiwemo Ofisa Uhamiaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Sylvester Chambo na wanae wanne wamefariki dunia papohapo huku wengine wanane wakijeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari jingine Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro.
RPC wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema imetokea eneo la Saweni Wilaya ya Same,Mkoani Kilimanjaro.
Amesema gari lililoua Familia ya Watu 7 lenye usajili namba T.618 AWP aina ya Toyota Corola lilikuwa likitokea Mkoani Tanga kuelekea Moshi na kugongana uso kwa uso na gari T.515 DMV aina ya Volkswagen lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar es salaam na kusababisha majeruhi wanane.
"Chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva wa gari T.618 AWP Toyota Corola lililokuwa likiendeshwa na Ofisa Uhamiaji wa KIA kuhama upande wake wa kushoto wa Barabara na kuelekea upande wa kulia wa Barabara na kugongana uso kwa uso na gari T.515 DMV Voxywagen”