Ali Kamwe Amchana Mwinyi Zahera " Zahera sio Mwajiriwa wa Yanga Muda"



Ameandika Ali Kamwe:

Naheshimu sana wasifu wa Mwinyi Zahera.. Ni kocha mkubwa. Naheshimu pia maoni yake kama Mtaalam wa soka.

Lakini ndugu zangu Waandishi wa Habari nafikiri kuna jambo mnatakiwa kulifahamu.

Zahera sio mwajiriwa wa Yanga. Mkataba wake ulishamalizika tangu Septemba.

Akiwa Yanga, alikuwa na Cheo cha Mkurugenzi wa Maendeleo ya soka la vijana na Wanawake.

Nafikiri kwa kujenga zaidi, kabla Zahera hajaanza uchambuzi wake wa unene wa wachezaji, ni vyema mkaanza kwa kumuuliza kwenye majukumu yake.

Kwa nafasi yake, kwenye soka la vijana ameacha mafanikio gani kwa @yangasc?

Kwenye Soka la Wanawake pia kwa amefanya nini kwa @yangasc_princess ?

Changamoto gani alipata? Nini alifanya kama mtaalamu kuzitatua? Nafikiri haya ni maswala ya msingi kabisa ambayo Zahera anatakiwa kuulizwa na kuyajibia kwa sasa.

Narudia tena, Naheshimu maoni yake kama mtaalamu wa soka Lakini msiruhusu akaruka hatua muhimu.

Hii itasaidia wasikilizaji wenu na mashabiki wa soka kupata maarifa zaidi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad