Duniani kuna wabunifu wengi sana leo mfahamu Robert Heft aliyezaliwa mwaka 1941 mbunifu aliyebuni bendera ya Marekani mwaka 1958, akiwa na umri wa miaka 17 tu, kipindi hicho alikuwa bado mwanafunzi, ubunifu huo aliufanya darasani katika kazi waliyopewa na mwalimu wa somo la historia ya Marekani ndipo alifanikiwa kubuni Bendera iliyokuwa na nyota 50, baada ya kazi hiyo kukamilika mwalimu alimpatia alama B ambayo Robert hakuridhika nayo.
Kipindi hicho Rais wa Marekani alikuwa Dwight Eisenhower alikuwa ametoa agizo la bendera mbalimbali kupelekwa kwake ili aweze kuchagua bendera itakayofaa kutumiwa Marekani, kati ya bendera 1500 zilizomfikia Rais na ile ya Robert ilipelekwa, kutokana na kutoridhishwa na alama ambazo mwalimu alimpa Robert alimuhakikishia mwalimu kuwa bendera yake ni nzuri na ndio Rais ataichagua.
Baada ya kupelekwa kwa Rais kweli Bandera ya Robert iliyokuwa na nyota 50 ilipitishwa na kuchaguliwa na Rais itumike Marekani, baada ya hapo mwalimu aliamua kubadili matokeo na kumpatia Robert alama A tofauti na ile B aliyompa mwanzo
Nyota 50 aliziweka kwenye bendera hiyo kumaanisha majimbo ambayo yalikuwa yamejiunga na USA lakini hakuishia hapo, kabla hajafariki dunia mwaka 2009 alikuwa tayari amebuni bendera nyingine ya nyota 51 ambayo itatumika kama jimbo jingine litajiunga na USA.
.
.
Imeandikwa na @officialtinana