Florence Samwel ambaye ni mtumishi wa Wizara ya Kilimo amezishtaki Hospitali za TMJ na Hindu Mandal pamoja na Dkt. Maurice Mavura katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam baada ya uchunguzi aliofanyiwa katika Hospitali ya Apollo nchini India kutoa majibu tofauti na aliyopewa nchini.
Mlalamikaji huyo anadai fidia ya TZS milioni 500 kwa madhara aliyoyapata kutokana na makosa aliyofanyiwa na hospitali hizo ambapo anadai kuelezwa kuwa ana saratani na hata kuondolewa tezi moja, hivyo kulazimika kuishi kwa kutumia dawa maisha yake yote ilhali hana tatizo hilo.