Aua mke, baba yake mzazi na kumjeruhi kaka yake




Jesto Lucas (34), mkazi wa Kijiji cha Nyashoshi, Kata ya Buhumbi wilaya ya Magu mkoani Mwanza, amemuua Baba yake mzazi pamoja na aliyekuwa mke wake kwa kuwakata mapanga kisha na yeye mwenyewe kujinyonga kwa shuka, huku kisa kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Inadaiwa mwanaume huyo aliachana na aliyekuwa mke wake lakini bado alikuwa anampenda, na kwamba alitekeleza unyama huo baada ya mke wake huyo kwenda kumsalimia baba yake mkwe (Baba wa Jesto), na wakati anamcharanga mapanga Baba yake alishuhudia tukio hilo na ndipo alipoamua kuwaua wote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kisimo A John Misalaba, pamoja na Mtendaji wa Kijiji cha Nyashoshi Esther Peter, nao wakaeleza namna wanavyolifahamu tukio hilo na kuahidi kufanya mkutano wa hadhara kwa ajili ya kuweka ulinzi shirikishi wa namna ya kuwajengea uelewa wananchi wa kuishi vyema kwenye ndoa na mahusiano yao

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad