Baada ya Rayvanny Anayefuata Kuondoka WCB ni Mbosso Khan


Ninaamini kwamba Mbosso ndio atakuwa msanii namba nne kuondoka WCB, Diamond anapambana kuhakikisha Mbosso anakuwa msanii mkubwa, hii ni hatari, maana jinsi anavyokua pia uwezekano wa yeye kuondoka WCB unaongezeka.


Achana na Mavoko, Tumeona Harmonize alipokua tu Akachomoka, Rayvanny pia amechomoka, hivyo hivyo Mbosso atafuata.


Unaweza ukadhani kwamba Zuchu atachomoka mapema kabla ya Mbosso, hilo haiwezekani. Zuchu ana mapenzi makubwa dhidi ya Diamond Platnumz hivyo kuachana nae sio rahisi, pia ni kawaida kwa wanawake, huwa hawawezi kupambana zaidi, wakipata hela kidogo tu wanatulia pia sio rahisi kudanganywa kwamba waondoke kwenye Lebo.


WCB hivi sasa wameanza kuwekeza zaidi kwa Mbosso, Kuna E. P yake inatoka soon, Diamond amethibitisha hilo Baada ya ku-post clip akicheza moja ya ngoma inayopatikana katika E.P hiyo.


Mwezi Ujao Mbosso anafanya Tour Marekani. Hii imewahi kutokea kwa Rayvanny, mwaka 2018 akitamba na "Pochi nene" alifanya Tour UK na USA.


Kwa jinsi ambavyo WCB wanapambana kwa sasa kumkuza Mbosso kimataifa zaidi watambue pia kuwa siku za yeye kukaa hapo zinazidi kupungua.

By Hopetyga

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad