Baada ya Yanga Kuondolewa Mabingwa Sasa Kupambana Shirikisho





TIMU ya Yanga imeshindwa kutinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa pili wa marudiano uliopigwa Uwanja wa Al-Hilal Jijini Omdurman.

Bao hilo lilifungwa mapema tu dakika ya tatu kupitia kwa Mohamed Abdel Raman baada ya mabeki wa Yanga kufanya makosa na kuifanya timu hiyo kuondolewa kwa jumla ya mabao 2-1 kufuatia mechi ya kwanza ambayo ilifanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 8 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa timu hizo kufungana bao 1-1.

Licha ya Yanga kuonekana kucheza vizuri tangu mwanzo wa mchezo ila imeshindwa kuvunja rekodi yake ya miaka 24 ya kutinga hatua ya makundi kwenye michuano hiyo baada ya mara ya mwisho kufanya hivyo 1998.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara walianza kampeni zao vizuri katika michezo hii huku wakionekana wataleta ushindani mkubwa baada ya kuanza vyema hatua ya awali kwa kuiondosha Zalan FC ya Sudani Kusini kwa jumla ya mabao 9-0.


Kuondoshwa kwa Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kunaifanya rasmi timu hiyo kuanguka katika kombe la Shirikisho ambapo sasa itacheza na timu moja kwenye hatua ya mchujo ili kusaka nafasi ya kutinga makundi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad