Baba Levo "Mimi lazima Nimfukuze Mwanamke Yakimpata Kama ya Mkewe Masanja"




Baba Levo azungumzia skendo ya mkewe mchungaji Masanja Mkandamizaji

Msanii Baba Levo ametilia kwenye mizani sakata linaloendelea katika kanisa la mchungaji Masanja Mkandamizaji, baada ya katibu wa kanisa kujitoa uhai kisac kukataliwa kimapenzi na mke wa mchungaji huyo.

Levo ambaye alikuwa anazungumza na wanablogu alizungumzia suala hili kwa undani na kuonekana pia akimlaumu mkewe Masanja kwa kuwa na maongezi na yule katibu ambaye sasa ameshatangulia mbele za haki kwa kujiua.


Chawa huyo wa lebo ya Diamond Platnumz, WCB Wasafi alisema kuwa mkewe Masanja Mkandamizaji alifanya makossa ya kuendekeza mawasiliano na jamaa huyo na badala yake angemkataa moja kwa moja na hilo kukamilika.

“Wanawake wanatungiza kwenye majanga ambayo ni mazito. Polisi wanasema kweli kulikuwa na mawasiliano kati ya yule jamaa na mke wa Masanja, lakini mkewe mchungaji akamkataa jamaa. Unapomkataa mtu, mwanamke, mkatae moja kwa moja. Sema sitaki basi,” Baba Levo aliwashauri wanawake.

Alisema kuwa hata hivyo, Mchungaji Masanja alitekeleza wajibu wake kama mume na kubaki na mkewe ila akajizungumzia yeye kama Baba Levo kuwa suala kama hilo likimtokea hatofanya kitu kingine zaidi ya kumfukuza mwanamke tu!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad