Waziri Ummy atamani kubadilisha jina la hospitali ya Mirembe



Dodoma. Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amesema anatamani kubadilisha jina la Hospitali ya Magonjwa ya Akili la Mirembe kwasababu watu wanaoenda katika hospitali hiyo wanaonekana kama ni machizi.

Ummy ameyasema hayo leo Ijumaa Oktoba 28, 2022 wakati akizungumzia mapango wa mafunzo wa ubingwa bobezi kwa watumishi wa umma.

Amesema ameshamwelekeza mkurugenzi wa maendeleo ya mafunzo na raslimali watu kuhakikisha huduma za matibabu ya afya ya akili zinapatikana hadi ngazi ya chini.

“Tumekubaliana tutaanzisha kozi ya diploma kwa ajili ya wauguzi wa magonjwa wa afya ya akili, ilikuwepo zamani lakini ikafutwa.”


“Mpaka afike juu kule Muhimbili ama Mirembe, halafu Mirembe natamani hata nibadilishe jina la hospitali ya Mirembe unaonekana kuwa ni chizi, wewe una matatizo,” amesema.

Amesema afya ya akili ni tatizo ambalo linampata kila mtu na kufananisha na afya ya mwili ambapo watu hupata magonjwa mbalimbali ikiwemo mafua, kifua kinauma.

“Unaweza leo usiamke vizuri, mood imebadilika. Ni kama afya ya mwili inavyopata misukosuko na afya ya akili pia inapata misukosuko. Tunataka wapate huduma yenye staha na kuheshimiwa utu wake,” amesema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad