Bongo Tafuta Jina tu, Mambo ya Usanii Yatakuja Yenyewe


Binafsi sikuwa najua kama Aggy baby nae ni msanii wa Bongofleva, tena ana mashabiki wengi

Nimekutana na ngoma yake huko inawekwa kwenye kundi moja la shutuma za copyright issues pamoja na ngoma mpya ya nandy “Mchumba"

Siku si nyingi pia mwanamitandao “Tuerny" aliachia ngoma yake ya kwanza kuashiria kuingia rasmi kwenye muziki na ali/ame/anapewa airtime kubwa sana na Media

Karibu Tanzania, Nchii pekee ambayo mtu akiwa na jina kidogo tu anaingia kwenye filamu, muziki, fashion nk... huku vipaji halisi vinaachwa mtaani viendelee kupotea

Ifike mahali kuwe na vigezo vya mtu kutambulika kama mwanamuziki kama kweli tunahitaji kuupeleka muziki wetu kwenye level kubwa zaidi ya kimataifa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad