Breaking News: Wanamuziki Killy na Cheed Watemwa Rasmi Konde Gang



Uongozi wa lebo ya muziki wa @kondegang umetoa taarifa kwa umma kuweka wazi makubaliano ya kusitisha mikataba na Wasanii wawili waliokuwa chini ya lebo hiyo @officialkilly_tz na @officialcheed.


“TAARIFA KWA UMMA


Uongozi wa Konde Music Wordwide Unachukua Fursa Hii

Kuutaarifu Umma Leo Tar 10/10/2022 Tumefikia Makubaliano Na Wasanii Tajwa Hapo Chini Ya Kusitisha Mkataba Kutokana Na Sababu Mbali Mbali

Zilizo Nje Ya Uwezo Wetu.


1.Ally Kili Omary Aka (Killy)

| 2.Rashid Daudi Mganga Aka (Cheed)


Kwa Hiyo,Wasanii Hawa Watakua Wasanii Huru Na Kuweza Kufanya Kazi Na-Kuingia Mkataba Na Kundi Au Mtu Yeyote Na Kuendeleza Kazi Zao, Kwani Tunaamini Ni Vijana Wasanii Wenye Uwezo Mkubwa Wa kufanikiwa Katika Safari Ya Muziki.


Aidha, Konde Music Worldwide Haitahusika Na Jambo Lolote Litakalohusisha Wasanii Hawa Kuanzia Tarehe Tajwa Hapo Juu.


Tunapenda Kuwashukuru Killy Na Cheed Kwa Ushirikiano Wao Katika

Kipindi Chote Cha Kuwa Pamoja na Tunawatakia Mafanikio Mema

Katika Kazi Zao Hapo Baadae.”



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad