Diamond Platnumz Amponza Mbosso, Wimbo wa Yataniua Yaondolewa Youtube



Siku moja baada ya msanii kutoka lebo ya WCB, Mbosso kuzindua EP yake aliyoipa jina la KHAN katika ufukwe wa Bahari Beach jijini Dar es Salaam, moja kati ya nyimbo sita zilizomo kwenye EP hiyo imeondolewa Youtube.

Ngoma iliyoondolewa, inaitwa YATANIUA ambayo Mbosso ameimba na bosi wake, Diamond Platnumz na hivyo kufanya ngoma zilizosalia YOUTUBE kuwa tano, Asalaam, Wayo, Shetani, Pole na Huyu Hapa.

Tangu kuzinduliwa kwa EP hiyo, kuliibuka mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, Diamond akituhumiwa kuigilizia nyimbo mbili kwenye kipande alichoimba katika wimbo huo.

Kipande cha kwanza anachodaiwa kukopi ni kutoka kwa msanii Asake wa Nigeria katika Wimbo wake wa Peace Be Unto You ambapo alichokibadilisha Diamond ni maneno tu lakini staili ya uimbaji inafanana kwa kila kitu na kipande hicho cha Asake.

Kipande cha pili ambacho Diamond anadaiwa kukopi, ni kutoka kwenye ngoma ya Adiwele kutoka kwa msanii wa Afrika Kusini, Young Stunna akiwa amewashirikisha Kabza De Small na DJ Maphorisa.

Bado haijafahamika ni nini sababu kubwa ya kuondolewa kwa ngoma hiyo ingawa gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii ni kwamba huenda wenye nyimbo zao wameuripoti wimbo huo kwa kukiuka sheria za hati miliki.

Licha ya kuondolewa Youtube, bado wimbo huo unaendelea kupatikana kwenye platforms nyingine kama Audiomac na Spotify.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad