Manara ame-share picha tatu za tukio hilo akiwa katika hoteli ya Hyatt Kenpinsk, ambapo anaonekana ni mwenye furaha huku tabasamu likitawala katika uso wake. Pia wake zake wanaonekana wenye furaha iliyopitiliza wakiwa na mume wao kipenzi.
Kati ya mastaa waliotoa komenti zao kwenye post hiyo ya Manara ni pamoja na mwanamuziki @diamondplatnumz ambaye yeye huenda OUT hiyo ya Haji na wake zake imemkosha vilivyo, amesisitiza msimamo wake wa kuoa hivi karibuni, ikiwa ni mara ya pili anaeleza hilo katika posti ya Haji Manara.
"Nasisitizaje, niko njiani Babaaaa... 🙌" - ameandika Diamond.
Aidha, Babu Tale ambaye ni meneja wake, ameijibu komenti hiyo ya Diamond kwa kumwambia kama kweli anajiweza afanye hivyo alivyofanya Haji Manara.