Diamond Platnumz na Rekodi ya Tuhuma Nyingi zaidi za Uwizi wa Nyimbo za Watu


Imeaminishwa kuwa ukimuongelea #Diamondplatnumz basi unatafuta kiki, huu ni upofu ambao unaishi kwenye watu wenye uwezo wa kuona. Diamond anashikilia rekodi ya kuwa ndiye msanii aliyetuhumiwa zaidi kwenye uwizi wa kazi za wasanii wenzie hapa nchini. Kipindi anatoka akiwa na nyimbo mbili tu radioni, yani Kamwambie na Mbagala tayari jinamizi la uwizi likawa kama kivuli chake kwenye mwanga, msanii Tanzanite akaibua tuhuma za kuibiwa wimbo wake wa Uchawi na Wanga ambao melody yake ni Mbagala ya Diamond.


Jamaa alikomaa hadi Diamond akaona isiwe noma acha ampooze kwa kolabo, wakatoa wimbo unaitwa #Mapenzibidhaa, baada ya Hapo Tanzanite akala mute. Haikuwa muda mrefu sana, Diamond akanasa tena kwenye tego la Nataka kulewa, Pasha na Tundaman wakamkalia kooni kwa kuiba wimbo wao wa Amekua, H. Baba pia akilalamika kuibiwa. Huku na Huku mwamba akaingia kwenye 18 za msanii Wababa, akimtuhumu Diamond kwa kumuibia wimbo wake wa kitorondo na kuugeuza jina tu, Mdogo mdogo.


No.1 ya Diamond ilikuwa ni Ngoma ya Dayna Nyange (Kwa mujibu wa Dayna) na ilikuwa itoke kama kolabo, Dayna Ft Diamond, ila mwamba akamzunguka Dayna, Shedy Clever akachezesha Dish ngoma ikawa ya Diamond. Orodha ni ndefu kiasi kwamba unashindwa kuelewa tatizo la Diamond ni nini, alianza kunyatia idea za watu hapa nyumbani na sasa kahamia kimataifa, anaishia kukutana na fedhea ndogo ndogo.


Imagine ndani ya mwezi mmoja wasanii watatu wa label moja kubwa nchini wanatuhumiwa kwa uwizi wa nyimbo. Ilianza kwikwi ya Zuchu, na sasa ni #yataniua ya Diamond na Mbosso iliyoshushwa YouTube hii leo October 29 kwa tuhuma za hakimiliki, ikiwa ni hivi karibuni wimbo wa naanzaje,Gidi zikituhumiwa kukopiwa. Mwanzoni ilionekana kama kawaida ila sasa imekuwa too much, alafu utasikia mashabiki wakikwambia hamna kitu kipya ,vyote ni marudio😀, nchi ngumu sana hii ankali.


#sajomedia

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad