Edo Kumwembe: Nasreddine Nabi alijinyonga mwenyewe




Mwandishi wa Habari za Michezo Mwandamizi nchini Tanzania Edo Kumwembe, anaamini Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi hakuzipanga vizuri karata zake kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Kumwembe ambaye kwa sasa amejikita kwenye uchambuzi wa Soka ametoa kauli hiyo akiwa kwenye Kipindi cha Sports Arena cha Wasafi FM mapema leo Jumatatu (Oktoba 10) asubuhi kwa kusema, Kocha huyo hakukipanga vizuri kikosi chake Jumamosi (Oktoba 08).

Kumwembe amesema anaamini kuwapanga kwa pamoja viungo Aziz Ki na Feisal Salum ‘Fei Toto’ lilikua kosa kubwa kwa Kocha Nabi, kwani alidhihirisha kulazimisha mfumo wa kuwatumia wawili hao, ambao haukufanikiwa.

Lingine ambalo Mkongwe huyo ameliona na kuamini huenda liliikwamisha Young Africans kwenye mchezo huo, ni kushindwa kutumika ipasavyo kwa Yannick Bangala katika neo la Kiungo na badala yake alitumiwa kama Beki wa Kati.


“Kuwatumia wote (Aziz Ki & Fei) kocha alilazimisha na haikulipa, kwanza Aziz Ki hayuko Form, hayuko vizuri, wakati mechi inaendelea nilikuwa nafikiria Aziz Ki atoke aingie labda Mwanyeto, Bangala asogee kwa Aucho, Fei asogee mbele kwa Aziz Ki,” amesema Edo Kumwembe

Hata hivyo Young Africans bado wana nafasi ya kurekebisha makosa hayo ya kiufundi watakapocheza mchezo wa Mkondo wa pili Jumamosi (Oktoba 15) ugenini Sudan.

Katika mchezo huo Young Africans ikitakiwa kusaka ushindi wa aina yoyote ama sare kuanzia 2-2, ili kujihakikishia nafasi ya kutinga Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad