Fahamu wanaume waliotoka kimapenzi na Wema Sepetu kabla ya Whozu







Ni wazi kuwa kwa sasa muigizaji maarufu wa Bongo Wema Sepetu anaogelea kwenye dibwi kubwa la mahaba.

Mlimbwende huyo mwenye umri wa miaka 32 alitangaza mahusiano yake mapya na Whozu mnamo siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake. Wawili hao wamekuwa wakichumbiana kwa muda ila hawakuwahi kufichua.

"Kwa muda mrefu nimekuwa sina raha. Nimekuwana huzuni, nimekuwa  nikilia lakini tangu nilipokutana na Chibaba wangu (Whozu) nimekuwa na raha na amekuwa akiweka tabasamu kwenye uso wangu," Wema alisema katika video ya moja kwa moja iliyopeperushwa kwenye YouTube usiku wa kuamkia Jumatano.

Wema na Whozu wamekuwa wakijificha chini ya 'urafiki' hadi hatimaye kufikia kufichua mahusiao yao.

Whozu hata hivyo sio mwanaume wa kwanza kuwa katika maisha ya muigizaji huyo. Hapa chini tunaangazia baadhi ya wanaume ambao amewahi kuchumbiana nao katika miaka ya awali.


1. Steven Kanumba

Miaka kadhaa iliyopita Wema aliwahi kufichua kuwa marehemu Steven Kanumba ndiye alikuwa mpenzi wake wa kwanza wa kweli.

Wema alichumbiana na muigizaji huyo kwa muda kabla ya kukumbana na kifo chake mwongo mmoja uliopita. Wakati huo alikuwa kijana mdogo tu aliyekuwa akijenga taaluma yake ya uigizaji.

2. TID

Miaka kadhaa kabla ya kukutana na Kanumba, Wema alichumbiana kwa muda na mwimbaji wa Bonge mkongwe TID

Wawili hao walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mwaka wa 2006 wakati Wema alipokuwa Miss Tanzania.

3. Diamond Platnumz

Wema Sepetu na staa wa Bongo Diamond Platnumz walichumbiana kwa kipindi kirefu kabla ya mahusiano yao kufika kikomo mwaka wa 2014.

Wasanii hao walikuwa kwenye mahusiano ya msimu yaliyokumbwa na madai kadhaa ya kuchepuka. Hata hivyo waliendelea kuchumbiana hadi Diamond alipokutana na Zari na hatimaye kumtema muigizaji huyo.

4. Luis Munana

Wema alikutana na mwanamitindo wa Namibia Luis Munana takriban mwaka moja baada ya kutengana na Diamond.

Baada ya kipindi kifupi alitengana naye kwa sababu hakuweza kumudu uhusiano wao wa mbali na baadae akakutana na Iddris Sultan. 

5. Iddris Sultan

Wema alichumbiana kwa muda na muigizaji mwenzake Iddris Sultan kabla ya kutengana kwao mwaka wa 2016.


Licha ya mahusiano yao kugonga mwamba miaka mingi iliyopita wawili hao wamebaki kuwa marafiki wa karibu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad