Sakata la Harmonize na wasanii wake, Killy na Cheed, baraza la Sanaa Taifa (Basata) limewapa siku mbili kumaliza mambo waliyoafikiana katika mkataba wao. Tovuti ya Mwananchi imeripoti.
Ofisa Sanaa Mwandamizi wa Basata, Abel Ndaga amebainisha hayo baada ya kukaa katika kikao cha pili kilichopangwa kukutanisha pande zote mbili baada ya kikao cha kwanza kilichopangwa Oktoba 12, 2022 ambapo vikao vyote msanii Harmonize hakuweza kuhudhuria.
"Tumejadiliana vizuri kwenye kikao na kila kitu kimeenda sawa, tumewapa siku mbili waweke mambo sawa na kurudi hapa kwa kuwa kila kitu kwenye mkataba kinajieleza," ameeleza Ndaga akizungumza na gazeti la Mwananchi.
Hata hivyo, Ndaga alisema katika kikao hicho kijacho lazima Harmonize mwenyewe awepo na hawatahitaji kumuona tena mwakilishi kwa kuwa maamuzi yanaenda kutolewa rasmi.