Staa wa muziki wa Bongo Flava na Mmiliki wa Record Label ya @kondegang , @harmonize_tz ameweka wazi kutofanya lolote linalohusiana na kuipromote albamu yake mpya ya MADE FOR US inayo tarajiwa kutoka ijumaa hii ya tarehe 28/10.
Kupitia insta story yake, Konde Boy amedai hakuna Press conference, hakuna media tour, Billboards, wala Listening Party kuhusiana na MADE FOR US, sababu kubwa ni kuwa ameshafanya kila kitu studio, na hii ni albumu kwaajili ya watu wa Afrika mashariki na wale wanao ongea kiswahili duniani.