HARMONIZE MBWANA...ATINGA MAZOEZINI YANGA KUWAPA MOTISHA MECHI YA JUMAPILI


Mwanamuziki @harmonize_tz ambaye ni shabiki kindakindaki wa klabu ya Yanga, ametinga katika kambi ya klabu hiyo iliyopo Kigamboni Jijini Dar es salaam na kushuhudia mazoezi ya mwisho mwisho ya klabu yake pendwa kuelekea kwenye mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba Jumapili hii ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara (NBC).


Mtanange huo utapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa, kuanzia majira ya SAA 11 jioni huku wenyeji wa mchezo huo wakiwa ni Yanga.


Akiwa kambini huko, @harmonize_tz pia amekutana na Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said. Unaionaje hii love ya Konde Boy kwa klabu yake pendwa anayoishabikia @yangasc

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad