Harmonize ni Mpambanaji na Mfano wa Kuingwa Kimuziki



Tangu kutoka katika rekodi lebo ambayo ilikuwa inamsimamia Harmonize amekuwa akiangaliwa ni sehemu gani atafika katika muziki wake.

Wengi walimtupia macho na kuamini huenda ataishia njiani au atashuka kimuziki baada ya kuanza kufanya kazi mwenyewe.

Harmonize wa 'Uno' mpaka wa 'Leave Me Alone' amekuwa na mapito mengi ya kuhakikisha anaisimamisha vilivyo brandi yake katika muziki.

Kazi baada ya kazi ndio kitu pekee ambacho kimeweza kumsimamisha Harmonize mpaka kufikia alipo sasa.

Na kwa mujibu wa mtandao wa 'Google Trends' Harmonize ni mmoja wa wasanii nchini Tanzania anayefuatiliwa zaidi.

Kwa kuonyesha kuwa ni mpambanaji halisi kwa kipindi cha miaka miwili ametoa album mbili na yupo mbioni kutoa album ya tatu.

Album ya kwanza 'Afro East' aliitoa mwezi march 2020 album ya pili 'High School' aliiachia Novemba 2021, na album ya tatu 'Made for Us' ametangaza kuitoa rasmi Oktoba 28.

Album tatu kwa miaka mitatu katika muziki wa Bongo fleva sio kazi ndogo na inahitaji maandalizi makubwa huenda @harmonize_tz akawa ndiye msanii pekee aliyetoa album tatu mfululizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad