Hivi ndivyo Ukraine inashinda vita ya mitandao ya kijamii



Baada ya karibu miezi minane, vita vya Ukrane viko kwenye mizania sawa. Mashambulizi ya Ukraine yanaendelea kupiga hatua, wakati vikosi vya Urusi bado vinaendelea kusonga mbele kwenye sehemu zingine. Lakini kwenye mtandao, ni jambo la upande mmoja sana.

"Hili ni taifa la kukumbukwa," anasema Olena, mjasiriamali wa Kyiv ambaye anasimamia timu za watu waliojitolea kwenye mitandao ya kijamii.

"Ikiwa hii ilikuwa vita ya maigizo, tungekuwa tunashinda." Olena sio jina lake halisi. Kutokana na unyeti wa kazi anayoifanya yeye na timu zake kwa niaba ya wizara ya ulinzi ya Ukraine, ameomba kutotajwa jina.

Timu zake hufanya wakati wote, zikishughulikia taarifa kutoka kote nchini, zikitoa video za kusisimua, ambazo mara nyingi huwekwa kwenye muziki, kuwafikia walengwa ndani na nje ya nchi.

Kama vile Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anavyopanga hotuba kwa mabunge ya kigeni ili kuzingatia historia ya ndani, utamaduni na usikivu, vivyo hivyo pia timu ya kimataifa ya Olena yenye watu watano inafanya.

Video ya mwezi Juni iliyoishukuru Uingereza kwa usaidizi wake wa kijeshi iliangazia muziki wa Gustav Holst na The Clash, ukiwa na maono ya Shakespeare, David Bowie, Lewis Hamilton na mkusanyiko wa silaha za kupambana na vifaru zilizotolewa na Uingereza zikifanya kazi.

Olena anasema mojawapo ya video zake anazozipenda zaidi za "shukrani" ni ile iliyoisifu Sweden kwa uwekezaji wake wa thamani ya pesa nchini Ukraine: $20,000 (£17,900) silaza za mifumo ya roketi ya Carl Gustav, vinavyoweza kuangusha mizinga ya Urusi ya T-90 yenye thamani ya $4.5m.

Wimbo Ulikisia kwa maneo haya: Pesa za Abba, Pesa, Pesa.

Ukraine
Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa juhudi za timu hiyo, mtandao wa Twitter wa wizara ya ulinzi ya Ukraine sasa una wafuasi milioni 1.5 kote ulimwenguni.

Baadhi ya video zimetazamwa zaidi ya mara milioni moja. Video yao iliyofanikiwa zaidi, iliyotolewa mwezi wa Agosti baada ya mashambulizi kadhaa ya Urusi katika eneo la Crimea, imepata maoni ya mita 2.2.

Video hiyo ilikuwa inawadhihaki warusi kwa kwenda likizo kwenye peninsula na ilitumia wimbo wa Bananarama Cruel Summer.

"Wazo kuu ni kuzungumza na watazamaji wa kimataifa na kuonyesha kwamba Ukraine ina uwezo wa kushinda," anasema. "Kwa sababu hakuna mtu anataka kuwekeza katika hasara." Lakini timu nyingine ya Olena inatekeleza kazi ya uasi zaidi, iliyoundwa kuangazia hasara za Urusi na kuwakatisha tamaa wavamizi hao wa Ukraine.

UKRAINE
Chanzo cha picha, DEFENCE OF UKRAINE

Maelezo ya picha,
Video za Ukraine zinawaonya warusi kwamba watapasa hasara zaidi kwenye vita inayoendelea Ukraine

Huku video nyingi zinazoonyesha vikwazo vya kijeshi vya Urusi zikichapishwa kwenye mitandao ya kijamii, timu hiyo haina nyenzo nyingi. Lakini wamejifunza kupitia majaribio na makosa ni nini kinachofanya kazi na kisichofanya kazi.

"Tulianza kuonyesha maiti za Warusi," Olena anasema. "Na ndipo tukagundua kwamba kwa kweli haikufanya kazi. Iliwaunganisha zaidi dhidi yetu." Kisha timu hiyo ilijaribu kuonyesha picha za raia wa Ukraine waliokufa. Tena, ilionekana kutofanya kazi. "Tuligundua walikuwa wanajivunia jambo hilo. Hawakuwa wakikemea jambo hili hata kidogo," anasema. "Tuligundua kuwa lazima tufanye hivi kwa njia ya kisasa zaidi."

Ni vigumu sana kupima matokeo ya yanayotokana na kazi hii, lakini uhamasishaji wa hivi majuzi wa Vladimir Putin umewapa wanaojitoleanyenzo nyingi za kufanya kazi nazo. "Tulikuwa tukingoja uhamasishaji," Olena anasema. "Tulijua kuwa ingewavunja moyo sana."

Crimea Bridge
Chanzo cha picha, AFP

Kazi ya timu ya wizara hii ni moja tu lakini wapo watu wengi wa Ukraine wanaojitolea kutoa taarifa tena kwa haraka.

Akaunti za mtandao wa Telegraph huvutia idadi kubwa ya wafuasi. Moja, inayoitwa "Ukrainian Offensive", ina wafuasi 96,485. Kauli mbiu yake ni "kupigana kwenye mstari wa mbele wa vita vya habari tangu 2014."

Inatoa taarifa mpya za kijeshi, yanayoendelea Moscow na kupitia mara kwa mara matangazo ya vyombo vya habari vya Magharibi (ikiwa ni pamoja na BBC).

Kama vituo vingine vingi, haiepuki kuonyesha mateso, ikiwa ni pamoja na picha za wanajeshi wa Urusi waliokufa au wanaokufa. Mlipuko wa hivi majuzi kwenye Daraja la Kerch la Urusi, linalounganisha Urusi na Crimea inayokaliwa, uliibua wimbi kubwa la video, vichekesho huku jeshi la mtandao la Ukraine likiadhimisha kwa fujo.

Lakini nchi haikugeuka kuwa taifa la ninja za kidijitali mara moja. Miaka minane ya vita katika eneo la mashariki la Donbas imewapa watu muda mwingi wa kuboresha ujuzi wao, kutoka kukabiliana na taarifa potofu hadi kusambaza maudhui ya ucheshi yaliyoundwa ili kuongeza ari.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad