Je kuna uhusiano gani kati ya kuamka mapema asubuhi na mafanikio?




Kuna msemo usemao ''Kulala Mapema na kuamka mapema humfanya mtu kuwa na afya njema, tajiri na mwenye hekima'... Pia Kuna msemo 'kuamka mapema, hukupa maarifa, afya, utajiri'. Popote unapokwenda duniani, unapata ushauri huu.

Ni sawa kama ni ushauri au 'msemo', lakini je ukweli kuna jambo kama hilo?

Tim Powell, anayeishi Uingereza, kwa kweli huchukia kuamka asubuhi. Lakini anaamka kabla ya saa kumi na mbili asubuhi kila siku kwenda sehemu za kufanyia.

Usipande mlima siku ya kwanza
Anajiandaa kwenda kazini, anafika ofisini kabla ya kazi kuanza saa tatu asubuhi. Pia hutembea katika bustani karibu na ofisi kabla ya kuanza kazi.

Siku za Alhamisi, yeye huamka saa kumi na moja na dakika ishirini asubuhi kwa sababu inambidi kuhudhuria darasa la lugha ya Kijerumani kabla ya kwenda kazini.

Tim Powell anafanya kazi saa 70 kwa wiki. Yeye ni wakili anayeshughulikia madai yanayohusiana na hati miliki. Wanapaswa kuamka asubuhi na mapema kutokana na kazi. Ikiwa hawataamka mapema asubuhi, hawatapata muda wa kufanya mambo mengine maishani.


Ingawa alikuwa anaamka mapema kila asubuhi, ilikuwa vigumu sana kwake kujiingiza katika tabia ya kulala sana.

Anasema, "Hapo awali, baada ya kuamka asubuhi na mapema, nilikuwa nikihisi uvivu kwa muda mrefu. Mara nyingi nililala tena. Ikawa tabia baada ya muda."

Usifikirie kupanda Everest siku ya kwanza, anasema.

Watu wengi waliofanikiwa humaliza kazi zao muhimu mapema asubuhi bila bugudha yoyote.

Siku ya Anna Wintour, mhariri wa gazeti maarufu la Vogue, huanza saa kumi na moja na nusu asubuhi. Hucheza tenisi kwa saa moja kabla ya kuanza kazi.

Jinsi ya kuamka mapema asubuhi?
Wataalamu wana maoni kuwa muda wa kuamka asubuhi hadi kufika ofisini ni muhimu. Kazi nyingi binafsi ambazo hazihusiani na ofisi lakini muhimu zinaweza kufanywa wakati huu.

Lakini sasa swali ni jinsi ya kuzoea kuamka asubuhi na mapema?

Kulingana na Profesa Martin Hagar wa Chuo Kikuu cha Perth huko Australia, utaratibu wetu ni muhimu sana na utaratibu huu unategemea mazoea yetu binafsi.

Hagar anatafiti jinsi watu wanavyoweza kudhibiti tabia zao.

Anaamini kwamba tukiboresha ratiba zetu, mazoea yetu pia yataboreka.

Anaamini kwamba ikiwa utaratibu huo utaboreshwa, hata watu wanaofanya kazi usiku sana wanaweza kuamka asubuhi na mapema.

Hagar alijaribu kutumia uzoefu wake mwenyewe. Anaamka saa kumi na mbili asubuhi, anaenda kwenye mazoezi, anapata kifungua kinywa chenye lishe. Hata baada ya kufanya hivyo, aliweza kufika ofisini saa mbili asubuhi.

Kama ataruka kufanya mazoezi asubuhi, anaweza kukosa nguvu ya kufanya mazoezi baadaye jioni. Ili kuepusha hili, anaenda kulala ili kujiandaa kuamka asubuhi na mapema.

Wataalam wanahisi kuwa hakuna sheria maalum ya kuamka mapema asubuhi.

Wakati wako wa asubuhi
Jinsi ya kuanza asubuhi inategemea na mtu. Kwa sababu ratiba ya kila mtu ni tofauti. Wataalam wanahisi kuwa malengo na mtindo wa maisha wa kila mtu ni tofauti, kwa hivyo utaratibu hubadilika kutegemea na muhusika.

Swali kuu ni jinsi ya kupata muda nje ya ratiba yako asubuhi?

Ikiwa umechoka kuamka mapema asubuhi, weka kengele mapema kidogo kila asubuhi. Hatua kwa hatua hutengeneza tabia na ratiba ya kuamka mapema asubuhi.

Laura Vanderkam, mwandishi wa kitabu cha What the Most Successful People Do Before Breakfast, anasema, “Asubuhi ni yako, na hakuna mtu anayeweza kuiondoa kutoka kwako.

"Unaweza kushughulikia majukumu mengine wakati mwingine wa siku, lakini hifadhi asubuhi kwa ajili yako," anasema.

Vanderkam anatafiti kwa karibu taratibu na ratiba za watu waliofaulu na wenye shughuli nyingi.

Katika uchunguzi wake aligundua watu waliofanikiwa hutumia wakati wa asubuhi peke yake. Baadhi ya watu hawa wana nia ya kuboresha afya wakati wengine wana hamu ya kujifunza mambo mapya.

Ikiwa unataka kufanya kitu na huna muda wa hilo, jaribu kufanya asubuhi, anapendekeza Vanderkam.

Ili kuongeza ubunifu
Unapaswa kulala mapema ili kuamka mapema asubuhi. Hiyo inamaanisha kuwa hautapoteza muda wako wa jioni kwenye TV na mtandao.

"Kama vile wanaoamka mapema wanavyofaidika na muda, wanaolala kwa kuchelewa usiku zaidi wanaweza kufaidika na utaratibu wa asubuhi," anasema Marike Veith, profesa msaidizi katika Chuo cha Albion huko Michigan, Marekani.


Utafiti wao uligundua wanaochelewa kulala na kulala usiku wa manane walikuwa wabunifu zaidi asubuhi.

Chuo Kikuu cha Jimbo la Florida Prof. Roy Bamister anasema, "Kuamka asubuhi na mapema ni njia nzuri ya kukabiliana na matatizo kazini."

Anasema "Asubuhi utashi wetu unakuwa na nguvu zaidi, kwa msaada wake unaweza kukabiliana na changamoto nyingi. Hivyo watu waliofanikiwa hutumia muda wa asubuhi kwa busara."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad