Jeshi la Polisi Nchini Kupitia Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya (Ant drug Unit) kwa kushirikiana na Polisi Mikoa yote Tanzania bara na visiwani limeendelea kufanya Operesheni na Doria pomoja na Misako katika maeneo mbalimbali hapa nchini dhidi ya uhalifu na Wahalifu wa dawa za kulevya.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa Kitengo cha kuzuia dawa za kulevya Nchini Makao Makuu ya Upelelezi kamishina msaidizi wa Polisi ACP AMON KAKWALE amesema kuwa Jeshi hilo liliendesha opersheni Nchi nzima kuanzia Septemba 01 2022 hadi octoba 25 ambapo watuhumiwa 1,212 walikamatwa na kufungua kesi 1,030.
ACP Kakwale amebainisha kuwa kiasi cha dawa za kulevya kilicho kamatwa kwa kipindi hicho ni Bhangi Kg. 1962.154 sawa na Tani 1.96, Mirungi Kg. 1081.73 sawa na Tani 1.08 Heroin Gram 448.74 pamoja na kuteketeza mashamba ya bhangi hekari 9.55 na Miche ya Mirungi ipatayo 220.
Kakwale ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi za baadhi ya watu wachache wanaojihusisha na biashara haramu na matumizi ya madawa ya kulevya ili wachukuliwa hatua kali za kisheria.
Pia amevishukuru vyombo vya Habari katika kuelimisha na kutoa elimu juu ya athari ya dawa za kulevya ambayo yamekuwa yakiharibu nguvu kazi ya Taifa.