Wanajeshi waliosajiliwa wamelalamika kwa familia zao kwamba wamekuwa wakinywa pombe kupita kiasia
Tangu mwanzo wa usajili wa wanajeshi wa ziada nchini Urusi ,takriban wanajeshi hao 14 wamefariki – tunazungumzia kuhusu wanajeshi walioshindwa kufika mstari wa mbele wa vita na kuaga dunia kutokana na sababu tofauti katika vituo vya mafunzo na kambi za kijeshi .
Habari kuhusu waliofariki huonekana katika vyombo vya habari vya majimbo ya Urusi , ambapo ndugu za marafiki huwasilisha maombi. Mamlaka hatahivyo imekataa kuzungumzia kuhusu visa hivyo na lawama huwekewa waathiriwa wenyewe.
BBC ilifanikiwa kupata ripoti moja ya uchunguzi wa uhalifu iliozungumzia kuhusu sababu ya vifo hivyo huko Tyumen. Hatahivyo wale waliohusika katika uchunguzi huo hawajulikani.
Katika matukio zaidi , wachunguzi walianza na vyanzo vya vifo vya wanajeshi waliosajiliwa. Siku ya Jumatano wiki iliopita, msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov alisema kwamba makosa wakati wa usajili wa wanajeshi wa ziada yalionekana na wengi.
“Putin alisema kwamba iwapo hatungefanya hilo , tusingefahamu matatizo yaliokuwepo . Hivyobasi , hatua itachukuliwa kuhakikisha kuwa mfumo huo unafuata sheria,” Peskov aliongezea.
BBC ilikusanya maelezo kuhusu vyanzo vya vifo vyao kote Urusi.
Kisa cha kwanza zaidi kinachojulikana kuhusu vifo vya wanajeshi waliosajili hivi karibuni kilitokea tarehe 27 Septemba katika eneo la kabardino – Balkaria , ambapo mkaazi wa Kijiji cha Zvedny Boris Shavaev alifariki katika gwaride la kijeshi katika kambi ya kijeshi. Sababu ya kifo hicho ilitajwa kuwa mgando wa damu katika mishipa.
Tarehe 28 Septemba , mwanajeshi aliyesajiliwa katika eneo la Andreevsky karibu na Tyumen , alifariki kulingana na vyombo vya Habari . Mamlaka katika eneo hilo hayakutoa maelezo yoyote na haikuzungumza na vyombo vya Habari kuhusu tukio hilo.
Oktoba 11 , idara ya kijeshi inayohusika na uchunguzaji katika kambi ya kijeshi ya Tyumen ilisema kwamba uchunguzi wa keshi wa uhalifu huo umeanzishwa kuhusiana na kifo cha mwanajeshi mmoja lakini hakuna maelezo yaliotolewa.
Hatahivyo siku ya Jumatano chanzo kimoja kiliripoti kwamba mtu huyo mwenye umri wa miaka 49 alikuwa akifanya kazi ya nyumbani katika kituo cha huduma za kijamii . Mwili uliokuwa uchi ulipewa wanakijiji na cheti chake kilichotiwa Saini ya Asphyxia. Sababu ya kifo chake sio kujiua bali sababu nyengine , chanzo hicho kilisema.
Chanzo cha picha, Yevgeny and Tass
.
Maelezo ya picha, Katika viwanja vya mafunzo, wanajeshi wapya wanafunzwa jinsi ya kushughulikia silaha na kutoa huduma ya kwanza
Tarehe 28 Septemba , mwili wa mwanamume pia ulipatikana katika kitengo kimoja cha jeshi kusini mashariki mwa eneo la Trans=Baikal chombo cha Habari cha Chita.ru kiliripoti. Chanzo cha kifo kilithibitishwa na waandishi katika kamati ya uchunguzi ya jeshi la Uingereza , lakini hakuna maelezo zaidi yaliopatikana.
Tarehe 3 mwezi Oktoba , mtu mmoja aliripotiwa kufariki katika kambi ya kijeshi ya Novosibirsk Higher Military Command School. Habari kuhusu tukio hilo zilithibitishwa na kamishna kuhusu haki za kibinadamu katika jimbo la Novosibirsk Nina Shalabaeva. Kulinga na kamishna huyo ,mtu huyo alifariki akiwa usingizini.
Baadaye afisi ya mlalamishi, ilisema kwamba marehemu alikuwa mtu mwenye umri wa miaka thelathini na tano kutoka Bratsk, Alexander Koltun. Chanzo cha kifo cha Koltun katika ripoti ya matibabu ni kwamba alifariki kutokana na mshtuko wa moyo. Hatahivyo familia ya Koltun inashuku kwamba chanzo cha kifo cha mwanao kilikuwa kupigwa. Wanafamilia waliambia wanahabari kwamba baadhi ya mifupa ya marehemu ilikuwa imevunjika.
Vilevile mamake Koltun alisema kwamba mwanawe alilalamika kwamba walikuwa wakiuza pombe aina ya Vodka wakati waliposajiliwa. Anasema kwamba walikuwa wakitembea kila mahali kila mtu alikuwa anakunywa pombe , hawakupewa magwanda ya kazi , hawakupewa chakula , aliongezea, kwasasa walikuwa wanakula chakula walichobeba kutoka nyumbani, alinukuliwa na chombo cha Habari cha Sibir. Realii.
Tarehe 3 Oktoba , vifo vya wanajeshi watatu wa zaida waliosajiliwa katika jimbo la Sverdlovsk vilibainika. Wawili walifariki katika kambi ya mafunzo ya kijeshi ya Yelansky katika Kijiji cha Poroshino. Mwengine alifariki baada ya kuambiwa arudi nyumbani.
"Mmoja alifariki kutokana na shambulio na mwengine alijiua. Wa tatu alifutwa kazi na kuambiwa kurudi nyumbani ambapo alifariki kutokana na tatizo la ini , alielezea afisa wa serikali wa jimbo la Sverdlovsk Maxim Ivanov.
Hatahivyo siku hiyohiyo , vyombo vya Habari vilisema kwamba marehemu wa tatu aliyekuwa na umri wa miaka 44 kutoka Kijiji cha Chelyabinsk , Denis Kozlov , huenda alifariki kutokana na athari za vita vilivyozuka kati ya wanajeshi wa ziada waliosajiliwa na sio kutokana na tatizo la ini.
Mnamo Oktoba 4, vyombo vya habari viliripoti kifo cha raia aliyesajiliwa kutoka Krasnoyarsk Dmitry V. (jina kamili halijulikani) katika kitengo cha kijeshi cha Omsk.
Rafiki wa karibu wa Dmitry, ambaye walienda naye Omsk, alisema kwamba walitishiwa kwa sababu ya mzozo kati yao na wanajeshi wengine waliosajiliwa hivi majuzi..
"Tuna wasiwasi kuwa haikuwa yeye mwenyewe, kwa sababu Dima hakuwa na tabia ya kutaka kujiua, hakuna majaribio aliofanya. Ana watoto wawili wadogo. Wakati anaondoka, alikuwa salama na angerudi akiwa hai," Mkewe aliambia chapisho la NGS24.
Uchunguzi wa Kimatibabu utakuwa tayari baada ya mwezi mmoja na nusu, na Kamati ya Uchunguzi itawapa jamaa nakala ya ripoti ya uchunguzi huo wa maiti.
Mnamo Oktoba 5, mmoja wa waliosajiliwa alikufa katika uwanja wa mafunzo huko Penza wakati wa vipindi vya mafunzo, chombo cha habari cha PenzaInform kiliripoti. Jina la marehemu mwenye umri wa miaka 41 halijatangazwa.
Chanzo cha picha, Yevgeny and Tass
.
Maelezo ya picha, Wanajeshi wapya waliosajiliwa Urusi
Mnamo Oktoba 11, Elena Rogova, Kamishna wa Haki za Kibinadamu katika Mkoa wa Penza, alithibitisha kwa RBC kifo cha askari huyo aliyesajiliwa hivi karibuni.
Kulingana na afisi ya malalamishi, kwa mujibu wa data iliyopokelewa kutoka kwa kamanda wa kitengo cha jeshi, sababu ya kifo cha mtu huyo ilikuwa "tatizo la mojawapo ya viunge vyake vya mwili."
Hakutoa maelezo mengine yoyote, akimaanisha ukweli kwamba habari kuhusu wanajeshi wanaosajiliwa (pamoja na huduma ya kijeshi, kusafirishwa, mafunzo ya mapigano na usajili wao ni data ya kibinafsi ya wanajeshi) ambayo haifai kutolewa kwa umma.
Mnamo Oktoba 6, vyombo vya habari, vikitoa vyanzo, viliripoti kifo cha askari mwenye umri wa miaka 28 huko Kamenka, Mkoa wa Leningrad. Kulingana na Sirena na LenTV, alipata jeraha baya la risasi kwa kujipiga risasi kutoka kwa bunduki wakati wa mazoezi ya risasi.
Hakukuwa na maelezo mengine au maoni rasmi kuhusu tukio hilo.
Mnamo Oktoba 7, mwili wa mwanajeshi aliyesajilliwa ulipatikana katika Shule ya mafunzo ya Kijeshi la Novosibirsk. "Ndio, ni wawili tu sasa [pamoja na marehemu Alexander Koltun]. Sijui [kilichotokea], uchunguzi unaendelea," Shalabayeva alithibitisha.
"Wakati hatua za uchunguzi zinaendelea, ni wale tu wanaoziendesha wanaweza kueleza. hali iliwekwa wazi na baadhi ya mahitimisho yakatolewa.
Chombo cha habari cha Sibkrai kiliripoti kwamba askar wa pili alitoka Novosibirsk na, kulingana na jamaa zake, alikufa "kwa sababu ya vitendo vya ukatili." Jina lake halikutolewa.