Tarehe kama ya leo mwaka 2011 aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muammar Gaddaf alikamatwa na wanajeshi wa vikosi vya serikali ya mpito na baadaye akauawa.
Nikukumbushe kuwa Muammar Gaddaf, alikuja na wazo la mataifa ya Afrika kuungana, baada ya jitihada zake za kuunganisha mataifa ya Kiarabu kugonga mwamba.
Mwaka 2003 kwenye mkutano wa kumaliza mgogoro wa Israel na Palestina, bila kujali misimamo ya mataifa ya Kiarabu, Gaddaf alitoa wazo la mataifa hayo kuungana na kuwa taifa moja.
Lengo lilikuwa kuondoa mizozo ya ukanda wa Mashariki ya Kati, akipendekeza Israel na Palestina liwe taifa moja na lipewe jina kutokana na herufi za mwanzo za mataifa hayo.
Lakini jitihada hizo zilikwama na ndipo akaelekeza nguvu nyingi katika bara la Afrika, akiwaita 'kaka' Waafrika wote, lakini umauti ulimfika bila lengo lake hilo kutimia la Afrika kuungana na kuwa taifa moja.
Gaddaf ndiye kiongozi aliyekaa muda mrefu zaidi madarakani, katika bara la Afrika, tangu alipompindua Mfalme Idriss mwaka 1969.
Gaddafi alizaliwa mwaka 1942.