Kabla ya Kuachia Ngoma au Album Wasanii Wafanye Research

 

Kuna time zinatoka Album au Single mbovu kweli, unajiuliza hivi huyu muimbaji na Producer wake wana masikio kweli? Management ina kauli yoyote kwa msanii au inamuogopa msanii?


Mwisho wa siku nimegundua kwamba mganga hajigangi, ukiandaa ngoma yako usiisikilize wewe na watu wako wa karibu then mkaipitisha, siku zote kujihukumu huwa ni kazi sana, pia hata Watu wako wa karibu kutoa hukumu huwa ni vigumu sana, wengi huwa wanasema uongo tu, "oya umetisha, nakuona mbali", kumbe kiuhalisia ngoma/Album ni mbovu.


Ushauri wa Bure, ukitaka kutoa kazi yako, ingia mtaani ukafanye Research, tumia knowledge ya "Sampling", maana huwezi fanya research kwa population yote hii, Hivyo lazima uchague watu wachache ili kuwakilisha Wengi.


Utajua mwenyewe utatumia njia gani kutafuta hiyo sample, either utumie Probability au Non-Probability Sampling methods, cha msingi sample iwe na watu zaidi ya kumi, tena ambao hawana knowledge ya muziki maana hao ndio mashabiki huko mtaani, wao ndio wasikilizaji wakubwa wa kazi zenu huko mtaani.


Baada ya kuwapata waulize kazi yako wanaionaje, hapo ndio watakupa Comment za ukweli, then zifanyie kazi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad