Kamwe Usimsomeshe Binti wa Mtu Ili Uje Kumuoa...Utalia na Itakula Kwako



Wasichana hawataki kitu kizidi sana kwenye penzi. Ukimpenda saana anaboreka na kukuona dhaifu. Huna michepuko? Huisumbui akili yake? Wao hutaka hekaheka.

Wanapenda kitu ambacho hakipo. Adimu! Kisichopatikana kirahisi. Kitu cha kugombania. Ndo maana utaona muhuni ana nafasi kubwa ya kunasa wasichana wengi kuliko mtulivu.

Kwao ni rahisi kutoka na mume wa mtu kuliko 'singo boi'. Wanajiuliza kwanini upo 'singo'? Wanajipa jibu kuwa utakuwa huna maajabu. Ataenda kwa yule anakimbiliwa na wanawake.

Wapo wanaozidisha upendo na hisia za penzi. Hata kusomesha msichana, akisahau kuwa huyo siyo mke wake. Totozi zinazojielewa haziwezi kuwa na mtu wa hivi. Lazima zichomoe utambi.

Wanaamini mpaka jamaa kaamua kusomesha. Basi atamilikiwa kama mtumwa ndani ya nyumba. Matokeo yake anasoma huku akiwa na hofu, kuwa akimaliza anaenda utumwani.

Ndo maana matukio ya kusalitiwa na binti aliyemsomesha ni mengi. Acha kujitwisha jukumu la wazazi kwa kusomesha binti wa watu. Somesha mke au mama wa watoto wako siyo pisi za mjini.

Ajabu yule aliyesomesha anatemwa. Anapewa mtu ambaye hata nauli ya chuo asingeweza kutoa. Kwanini? Hamna lolote ni 'vikonfidensi' tu ndo vinampa mke. Yule aliyesomesha anatokea kikatili.

Hukatazwi kupenda. Lakini 'kontro' shobo. Unasomesha ili uoe badala ya kuoa ndipo usomeshe? Unaweza kusomesha kama msaada tu, lakini siyo kama akiba yako ya kuja kuoa. Utaumia tu.

Imeandikwa na: @blessed_tillah
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad