Kendrick Lamar ni Konyo, Ashinda Tuzo Sita BET Hip Hop Awards


Usiku wa kuamkia leo huko mjini Atlanta, Georgia nchini Marekani kulikuwa na ugawaji wa tuzo kubwa nchini humo za BET Hip Hop 2022, ikiwa ni msimu wake wa 17.


Habari njema kwa mashabiki wa rapa Kendrick Lamar, mkali huyo ameibuka na ushindi mnono kwa kukwara tuzo nyingi zaidi. Kendrick Lamar amefanikiwa kushinda jumla ya tuzo sita (6) za BET Hip Hop 2022.


Kendrick ameshinda katika vipengele vya Album Bora (Mr. Morale & the Big Steppers), Msanii Bora wa mwaka Hip hop, Mtumbuizaji Bora wa LIVE, Mwandishi Bora, Mwongozaji Bora wa Video akiwa na Davefree pamoja na Video Bora ya mwaka “Family Ties” akiwa na Baby Keem.


Hii ni REKODI ya aina yake kutoka kwa Kendrick Lamar ambaye amemgaragaza vilivyo rapa Drake aliyekuwa anawania takribani vipengele 14 vya tuzo hizo msimu huu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad