KIKOSI KAZI CHAPENDEKEZA UKOMO WA VITI MAALUM




Dar es Salaam. Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini, kimependekeza sheria ziboreshwe kuweka ukomo wa miaka 10 ya ubunge, uwakilishi au Diwani wa viti maalum

Akiwasilisha mapendekezo hayo leo Ijumaa Oktoba 21, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa kikosi kazi, Profesa Rwekaza Mukandala amesema wanapendekeza utaratibu wa kuwa na viti maalum vya wabunge wawakilishi na madiwani wanawake uendelee.

“Utaratibu wa kuwa na viti maalum vya wabunge, wawakilishi na madiwani wanawake uendelee isipokuwa sheria ziboreshwe kuweka ukomo wa miaka 10 kwa mtu kuwa mbunge mwakilishi, au diwani wa viti maalum, wakilishi huu ni njia ya kupata uzoefu na kisha kupisha wanawake wengine wenye nia ya kuongeza ujuzi masuala ya siasa na uongozi”


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad