Kikwete asimulia alivyopiga picha na Rihanna, "hawakunipa"




Rais mstaafu Jakaya Kikwete, leo amefanya mahojiano maalum na Clouds Media Group ambapo ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo suala la kukutana na staa wa muziki kutoka Marekani, Rihanna.

Kikwete amesema, alikutana naye na wakazungumza mambo mbalimbali kuhusu maisha yake aliyopitia kabla ya kuwa maarufu.

"Katika shughuli zangu za elimu nikiwa Marekani nilikutana na kundi la vijana wanamuziki kiongozi wao alikuwa Rihanna basi tukapataa wasaa wa kuzungumza, sema picha zangu hawajanipa bwana.Niliongea na yule binti maisha yake akanielezea jinsi alivyotoka kwenye familia masikini hadi kufanikiwa kwenye muziki,” alisema Kikwete.

Rais huyo Mstaafu leo Oktoba 7, 2022 alikuwa akiadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake akitimiza miaka 72 na Clouds Media Group kumfanyia mahojiano maalum.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad