Kiungo Mkabaji wa Simba SC Jonas Mkude akipambana na Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Stephen Aziz Ki
KLABU ya Simba SC inasubiri adhabu kutoka katika Bodi ya Ligi kwa sababu ya kufikisha kadi za njano tano (5) katika mchezo mmoja ambazo ni kinyume na kanuni.
Katika mchezo wa jana Jumapili, Oktoba 23, 2022, Derby ya Kariakoo, klabu ya Simba SC imepata kadi za njano tano huku watani wao wa jadi, klabu ya Yanga SC ikipata kadi za Njano nne (4).
Mwamuzi wa mchezo, Ramadhani Kayoko ametoa kadi za njano 9 kama ifuatavyo;
Okra Augustine (Simba)
Feisal Salum (Yanga)
Mzamiru Yassin (Simba)
Mohamed Hussein (Simba)
Khalid Aucho (Yanga)
Aziz Ki (Yanga)
Jonas Mkude (Simba)
Djuma Shabani (Yanga)
Habib Kyombo (Simba).
Klabu ya Simba kukumbwa na adhabu kutoka TFF
Kwa mujibu wa kanuni ya Ligi, klabu ikipata kadi za Njano tano au zaidi katika mchezo mmoja, klabu hiyo hutafsiriwa kuwa na utovu wa nidhamu.
Fahamu kwamba, kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, ni Bodi ya Ligi pekee ndio yenye mamlaka ya kutoa adhabu hiyo na si vinginevyo.
Mpaka kipenga cha mwisho, timu zote zimetoshana nguvu kwa kutoka sare ya kufungana bao 1-1. Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Augustine Okrah dakika 15 kabla ya Aziz Ki kuisawazishia Yanga kwa mkwaju wa adhabu dakika ya 45 ya mchezo.