Kocha wa Yanga Atamba Tutakwenda Sudan na Hesabu Tofauti



NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema baada ya kukamilisha dakika 90 za mwanzo Uwanja wa Mkapa, Dar, watawafuata Al Hilal kwao Sudan kwa mpango kazi tofauti.

Jana Jumamosi, Yanga ilicheza dhidi ya Al Hilal ukiwa ni mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Baada ya mchezo huo, timu hizo zinatarajiwa kurudiana wikiendi ijayo nchini Sudan.


Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi alisema: “Dakika 90 za mwanzo huwa ngumu na baada ya hapo inakuwa ni kwenye mchezo wa pili ugenini, tupo tayari na tutawafuata kwa mpango kazi mwingine kabisa.

“Wakiwa nyumbani wao watakuwa wanajiamini, hilo tunajua na sisi tunachohitaji ni kupata matokeo mazuri kwa kuwa nimeongea na wachezaji kuhusu umakini na kupunguza makosa kwenye eneo letu.”


STORI: LUNYAMADZO MLYUKA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad