Kwanini Xi Jinping kuwa kiongozi wa maisha wa China?



Chama tawala cha Kikomunisti cha China kinatarajiwa kumpatia muhula wa tatu wa miaka mitano Xi Jinping, ambaye anadai kuwa kiongozi mwenye mamlaka zaidi wa Uchina tangu nchi hiyo ilipotawaliwa na Mao Zedong katika miaka ya 1970.

Uamuzi - ambao unakuja baada ya ukomo wa mihula miwili kuondolewa katika mwaka 2018 - utaimarisha msimamo wake wa China.

Inawezekana kwamba Bwana Xi, mwenye umri wa miaka 69, ataendelea kuwa rais katika kipindi kilichosalia cha maisha yake.

Hatua hiyo ya kihistoria inatarajiwa kutolewa katika Kongamano la chama cha Kikomunisti litakalofanyika mjini Beijing tarehe 16 Oktoba - ukiwa ni mojawapo ya mikutano muhimu zaidi katika historia ya chama hicho.

Xi Jinping kwa sasa anashikilia nyadhifa tatu za juu:

Kama Katibu mkuu ndiye mkuu wa chama cha kikomunisti cha China. Kama rais ni mkuu wa taifa la Chima.
Kama mwenyekiti wa kamati kuu ya jeshi ni kamanda wa vikosi vya kijeshi vya nchi
Pia anaelezewa kam Mtu muhimu zaidi au Kingozi wa ngazi ya juu zaidi.
Bwana Xi ana uwezekano wa kuendelea kubakia na nyadhifa mbili, Katibu Mkuu wa chama na mkuu wa kamati Kuu ya jeshi katika kongamano kuu la chama - ambalo hufanyika kila baada ya miaka mitano - na urais katika Mkutano mkuu wa mwaka wa kitaifa wa watu wa China utakaofanyika utakaofanyika mwaka 2023.

Nini kinachofanyika katika kongamano?

Wajumbe wapatao 2,300 watakusanyika katika Tiananmen Square katika ukumbi wa Great Hall kwa karibu wiki moja.

Takriban 200 kati yao watachaguliwa kujiunga na kamati kuu ya chama pamoja na wajumbe mbadala wapatao 170.

Kamati kuu itachagua watu 25 kwa ajili ya kujiunga na ofisi ya chama. Na ofisi ya chama itawateua wajumbe wa kamati ya ofisi ya chama. Hawa ni wasomi wenye ujuzi na uwezo.

Kuna wajumbe saba kwa sasa, wakiwemo Katibu mkuu wa chama Xi Jinping. Wote ni wanaume.

Uteuzi wote haufanyiki katika kongamano lenyewe. Kamati kuu inatarajiwa kukutana siku moja baada ya kongamano kuu kumalizika.

Ni kwanini ni muhimu?

Bw Xi ataongoza uchumi wa pili kwa ukubwa zaidi duniani na mojawapo ya vikosi vikubwa zaidi vya kijeshi.

Baadhi ya wachambuzi wanasema ana uwezekano mkubwa zaidi wa kuishinikiza zaidi China kuchukua msimamo zaidi wa siasa ya kimabavu katika muhula wa tatu wa miaka mitano.

"China chini ya Xi inaelekea katika mwelekeo wa utawla wa kiimla," anasema Profesa Steve Tsang wa Chuo kikuu cha London cha mafunzo ya Uongozi na ya kiafrika (OAS).

"China chini ya utawala wa Mao ilikuwa na mfumo wa utawala wa kimabavu. Hatukuwa bado tumefika hapo, lakini tunaelekea katika mwelekeo huo "

G
Profesa Tsang anasema Kongamano linaweza kushuhudia mabadiliko ya katiba ya chama, ambapo " fikra ya Xi Jinping " inaonekana kama falsafa ya muongozo wa chama.

"Fikra ya Xi Jinping" ni nembo ya Bw Xi ya ujamaa wa Kichina, inayochukuliwa kama falsafa ya mtu anayelipenda taifa ambayo ni tofauti na haikubaliani na ubinafsi.

Chini ya uongozi wake mamlaka za Kichina zimeyafunga makampuni yenye nguvu katika sekta mbali mbali za uchumi.

"Iwapo hilo litatokea, watakuwa wamemfanya dikteta ," Profesa Tsang anasema.

Uongozi wa ngazi ya juu wa China, utakaofichukiwa katika kongamano ,utaweka viwango mbali mbali vya sera.

Kidokezo chochote cha muongozo wa China kitafuatiliwa kwa karibu kote duniani hususan kuhusu changamoto muhimu : kiuchumi, kidiploamasia na kimazingira.

Changamoto za kiuchumi za China

Uchumi wa China umeshamiri katika miongo ya hivi karibuni. Lakini kwa sasa inakabiliwa na kuvurugika kwa uchumi kulikotokana kufungwa kwa shughuli za kiuchumi kulikotokana na sheria za Covid, kupanda kwa bei ya za bidhaa na mzozo mkubwa wa mali.

Kuongezeka kwahofu ya kushuka kwa uchumi wa dunia kutokana na vita nchini Ukraine pia imeharibu imani.

Ukuaji wa uchumi chini ya uongozi wa Bw Xi ni wa kiwango cha chini kuliko chini ya marais wa awali Jiang Zemin na Hu Jintao.

China
Baadhi ya wachambuzi wanasema uhalali wa serikali ya kikomunisti unategemea zaidi uwezo wake wa kuleta mapato ya juu zaidi na kazi nzuri kwa ajili ya wafanyakazi wa kichina.

Utendaji mbaya wa kiuchumi wa miaka mitano ijayo unaweza kusababisha matatizo mabaya ya kisiasa kwa Bw Xi.

Kongamano litafanya mabadiliko muhimu ya vyeo vya wahusika muhimu katika ukuaji wa uchumi, mkiwemo gavana wa benki kuu na waziri mkuu.

Kumaliza kabisa Covid.

Mpango wa China wa kumaliza kabisa Covid ni moja ya sera muhimu za Xi. Wakati nchi nyingi za dunia zimerejea katika maisha ya kawaida, mamlaka za Uchina zimeimarisha juhudi zake katika kudhibiti milipuko, ikiwa na sheria ya kali za kudhibiti maambukizi, kuwapima watu wengi na vipindi virefu vya karantini.

Ripoti zinasema kuwa miji zaidi ya 70 ikiwemo miji ya Shenzen na Chengdu imekuwa chini ya sheria kamili za kudhibiti corona katika wiki za hivi karibuni, huku mamilioni ya wakazi wakiathiriwa, biashara nyingi zikivurugwa na kuna ripoti kwamba umma haujafurahiswa na hatua hizo.

G
Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,
Mhudumu wa matibabu akiwapima wakazi katika Guiyang, jimbo la Guizhou

Bw Xi ameapa "kupambana kabisa na maneno yoyote na vitendo ambavyo kupotosha , kuwa na wasi wasi au kukana" sera yake ya Covid. Mlipuko mkubwa kabla ya kongamano, au wakati wa mkutano wenyewe, unaweza kuchafua sura ya uwezo wa Bw Xi.

Baadhi ya wachambuzi wanasema chama kinaweza kutumia Kongamano kutangaza ushindi juu ya janga na kukamilika kwa sera ya kumaliza kabisa Covid.

Jambo jingine linaloweza kutokea, ni kwamba chama kinaweza kudai kuwa China - tofauti na nchi nyingine - inathamini maisha ya watu kuliko uchumi, na kutokana na hilo sera itandelea.

Taiwan na Magharibi

Bw Xi pia amependelea msimamo mkali kuhusiana na mahusiano na nchi za Magharibi, hususan kuhusu Taiwan.

Ziara ya Taiwan iliyofanywa na Spika wa Bunge la wawakilishi la Marekani katika mwezi Agosti iliifanya china kuanzisha mazoezi ya kijeshi, yaliyojumuisha kufyatuliwa kwa makombora, karibu na kisiwa hicho.

China inaiona taiwan kama jimbo lililojitenga ambalo hatimaye litakuwa chini ya udhibiti wa Beijing. Taiwan inajiona kama eneo tofauti na bara.

Bw Xi amesema "kuungana tena" na Taiwan "lazima kukamilike" kabla ya mwaka 2049, itakapotimia miaka 100 ya Jamuhuri ya watu wa China - na haijawahi kuacha uwezekano wa matumizi ya nguvu kufanikisha hili.

Wataalamu wa usalama wanasema kwamba kuchukuliwa kwa Taiwan na Uchina kutamaliza nguvu za Marekani katika Seeneo la magharibi mwa Bahari ya Pacific na zaidi.

Taiwan ni ya umuhimu kimkakati kwa magharibi, sehemu ya kile kinachoitwa "mnyororo wa kwanza wa kisiwa", eneo ambalo linajumuisha orodha ya maeneo ambayo yamekuwa na ushirika na marekani kwa miongo kadhaa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad