"Playboy", Album ya Fire Boy imetoka mwezi wa Nane. Katika Album hiyo utakutana na Ngoma inaitwa "Compromise", Fire Boy amemshirikisha Rema.
Imagine Fire Boy anatokea Lebo ya Olamide "YBNL NATION" ila ameweza kufanya Collabo na Rema ambaye anatoka "Jonzing World" ya kwake D'Prince, Lebo hii kitaalamu zaidi ni "Subsidiary/Tawi" la "Mavin records" ya kwake Don Jazzy.
Imagine ukubwa na Ushindani wa YBNL dhidi ya Jonzing/Mavin Records lakini wasanii wao wanafanya Collabo.
Hapa Tanzania huwezi kuona msanii wa WCB anafanya collabo na Msanii wa KONDE GANG/KINGS, WA KONDE GANG HAWEZI FANYA NA WCB/KINGS, WA KINGS HAWEZI KUFANYA NA WCB/KONDE GANG, nimeisahau NLM, ila na wao ni hivyo hivyo.
Inachekesha sana, wenzetu Lebo zinaanzishwa ili kukuza Muziki ila bongo lebo zinaanzishwa ili kuimalisha bifu na kukuza ile hali ya Umwamba, wao wanahisi kumiliki Lebo ni ufahari.
Kiukweli safari ya Maendeleo katika muziki kimataifa zaidi bado ni ndefu sana kama wabongo wakiendelea kuamini misimamo hii ya kimaskini, kijinga, kitoto, kishamba na kipuuzi.