Liverpool Hali Tete Ligi Kuu England, Kocha Klopp Kuchukua Maamuzi Magumu Kunusuru Timu



Mwalimu wa Liverpool, Jürgen Klopp ameahidi kufanya mabadiliko kadhaa kwa timu yake hiyo isiyoridhisha msimu huu akiamini Liverpool inahitaji kubadilika ndani ya uwanja.

Katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Rangers, Klopp alinukuliwa akisema, "tunatakiwa tujitahidi kuongeza nafasi bora zaidi na pia tupunguze makosa yanayotusababishia nyakati mbovu".

Klopp akizungumzia mabadiliko alisema, "kwa sasa hatuna muda sana, ila tunaweza kubadilika na kufanya vizuri zaidi, ikitupasa kubadilika tutafanya hivyo, ili iwe rahisi pia kwa wachezaji, hicho ndicho tunakifanya hivi sasa".

Pia kwa upande mwingine amemgusia mshambuliaji wake Darwin Nunez, akidai kijana bado anapambana sana kuyazoea mazingira mapya ndani ya Liverpool pamoja na ligi ya Uingereza.

Klopp akimzungumzia Darwin Nunez alisema, "uhalisia ni kwamba bado anazoea mazingira, daima mchezaji mpya humpasa kuzoea mazingira, wengi wanatamani kuona mchezaji mpya anafanikiwa haraka, huwa inatokea hivyo na kuna nyakati haiwi hivyo, Darwin anahitaji muda".
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad