Mashabiki wa Nandy Msijitoe Ufahamu Kuhusu Zuchu

 


Kuna muda Nandy akifananishwa na Zuchu, mashabiki wa Nandy wanakuja Juu na Wanadai kwamba Nandy asifananishwe na Zuchu maana Zuchu yupo kwenye Lebo ila Nandy anajisimamia mwenyewe.


Acheni kupotosha watu, Nandy ana management yake, anapata support kubwa kutoka Clouds, hakuna msanii wa kike bongo hii anayepata Support kubwa pale Clouds kama Nandy.


Pia mwaka 2021 Nandy ameingia mkataba na @empawaafrica, hii ni Kampuni ya @mreazi ndio inasimamia usambazaji wa kazi za Nandy, pia wanamlipia VIDEO zake nyingi, Empawa ndio imemtoa Joe Boy hivyo sio sehemu ya mchezo mchezo.


Hili suala la kusema Nandy hana support, anajisimamia mwenyewe life mara baada ya kusoma post hii.


Nandy anapitwa na Zuchu kutokana na jitahidi binafsi za Zuchu, wote wana Back up ila Effort Binafsi Wanatofautiana.


Watu wanakaza fuvu tu, Hizo support za Lebo, Management au Distribution Companies zina mchango mdogo sana katika Maendeleo ya msanii, kwa asilimia kubwa Maendeleo ya msanii yanategemea yeye mwenyewe.

By Hopetyga

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad