Wakati #georgsolti akiwa ndiye mwanamuziki mwenye tuzo nyingi zaidi za Grammy duniani (31) kwenye vipengele vya aina zote za muziki, #Jayz na #kanyewest wakiwa ndio wasanii pekee wa Rap/Hip-Hop duniani wenye tuzo nyingi zaidi za Grammy (21), kuna list pia ya mastaa wakubwa duniani ambao wamekuwa na bahati ya kuwa nominated mara nyingi kwenye tuzo hizo, ila bundi uwaandama kwenye kuzibeba, baadhi yao...
1. Snoop Dogg a.k.a Ankali Snoop amekuwa nominated mara 16 kwenye tuzo za Grammy nyuma ya R&B singer, Brian McKnight mwenye nominations 17 ambaye pia hajawahi kwara hata moja. Ankali alikuwa nominated kwa mara ya kwanza mwaka 1993, kama ilivyo kwa Brian McKnight, hadi leo wanasubiri ushindi wao wa kwanza.
2. Katy Perry amekuwa nominated mara 13 lakini hadi leo hajawahi onja ladha ya ushindi wa Grammy.
3.Busta Rhymes aliye mtunuku Diamond Platnumz jina la Michael Jackson wa Afrika, amekuwa nominated mara 12 tokea mwaka 1996 na bado hajui ladha ya ushindi wa Grammy. Mara ya mwisho kuwa nominated ilikuwa ni mwaka 2011 kwenye vipengele vya Best Rap Song na Best Rap Performance, vyote akipoteza mbele ya Kanye West.
4. Nicki Minaj, nominations 10 lakini ushindi 0, huku akipoteza mara 3 mbele ya Msanii mmoja, Kendrick Lamar.
5. 2pac Shakur, Nominations 6 ikiwemo moja baada ya kifo chake, ushindi 0, akiwa nominated kwa mara ya kwanza mwaka 1995 na kupoteza mbele ya Rapa Coolio ambaye pia amefariki mwezi uliopita, September 28, na Eminem.
6. Jenifer Lopez, Nominations 2 ushindi zero, akiwa nominated back to back, mwaka 2000 na 2001 kwenye kipengele cha Best Dance Recording.
Ukiachana hao ambao ndio mashuhuri zaidi kwa kizazi cha sasa, kuna Bjork, nominations 15 ushindi 0, Martina McBride (14), Dierks Bentley (14), Dianna Ross (12), Sia (9), Blake Shelton (8), Queens (4), The Beach Boys (4), Sammy Davis Jr (3), n.k