Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12, 2022, Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anne Makinda, amesema imekuwa ni utaratibu wa kimataifa kwamba baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu kazi zinazotakiwa kufanyika ni kuchakata matokeo ya Sensa na hatimaye kutoa matokeo ya sensa yenyewe
Mtakwimu Mkuu wa serikali Dkt Albina Chuwa, amesema mpaka sasa maandalizi ya kutangazwa kwa matokeo hayo yamekamilika na kinachofanyika kwa sasa ni taratibu ndogondogo za kuwezeaha kufanikisha tukio hilo kwani tangu awali wakishatangaza kwamba mwezi huu wa kumi ndio watatoa matokeo hayo
Kwa upande wake Kamisaa wa Sensa Tanzania visiwani Mohamed Salum Hamza, amesema Sensa hii imekuwa na mafanikio kutokana na kutumika kwa teknolojia ya hali ya juu tofauti na Sensa nyingine zilizofanyika nchini.