Mbappe "Taarifa ya kuondoka PSG hata mimi nimeshtuka, sijawahi kuomba kuondoka"


Mshambulizi Kylian Mbappe anasema “hakuwahi kuomba kuondoka” Paris St-Germain huku kukiwa na ripoti kwamba alitaka kuhama mji mkuu wa Ufaransa mwezi Januari. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 alitia saini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo mwezi Mei. Mbappe, mshindi wa Kombe la Dunia 2018, hapo awali alikuwa akihusishwa pakubwa na kuhamia Real Madrid. “Nina furaha sana,” Mbappe alisema baada ya kutengeneza bao la ushindi la Neymar katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Marseille Jumapili.


“Sijawahi kuomba kuondoka Januari.” anasema Mbappe Ripoti kwamba Mbappe alitaka kuondoka katika klabu hiyo ziliibuka kabla ya mechi ya PSG ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Benfica siku ya Jumanne.


“Sikuelewa kwa nini taarifa hiyo ilitoka siku ya mchezo. Nilishtuka kama kila mtu,” Mbappe alidai. “Watu wanaweza kufikiri nilihusika lakini sikuhusika kabisa.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad