Mchezaji Sopu Akiri Mambo ni Magumu Azam




MFUNGAJI Bora wa Michuano ya Kombe la ASFC, Abdul Suleiman ‘Sopu’ amekiri mambo magumu kwake kutokana na kushindwa kupenya kikosi cha kwanza cha timu hiyo iliyomsajili baada ya kuvutiwa na soka lake hasa kwenye fainali za ASFC akivaa uzi wa Coastal Union dhidi ya Yanga.

Sopu amesema kusajiliwa kwa mkwanja mrefu ni kama deni kwake kwani mashabiki wa klabu hiyo wangependa kumuona akiendelea kucheka na nyavu, jambo alilosema analifanyia kazi kwa kuongeza bidii na umakini pindi anapopata nafasi ya kucheza.

Katika nafasi yake ndani ya kikosi hicho wanashindania namba na Kipre Jr anayeonekana kupewa nafasi zaidi, Tape Edinho, Ayoub Lyanga, Tepsi Evance ambao wote ni vijana na wanataka kumshawishi Kocha Mkuu Denis Lavagne kuwapanga kikosi cha kwanza.

Sopu amekiri uwepo wa ushindani wa namba, ambao ameuchukulia kumuongezea maarifa zaidi kwenye utendaji wake, akiahidi kupambana kuhakikisha morali ya kucheka na nyavu inarejea.

“Ushindani upo kwa ajili ya kumjenga mchezaji kucheza kwa kiwango kikubwa, naufurahia kwani wote waliopo ni vijana wenye njaa ya mafanikio, hilo linanifanya nisibweteke bali nijue kuna kupambana kwa kila ari.

“Nilipata majeraha, naamini nikirejea nitafanya kazi kwa bidii kuhakikisha nakata kiu ya mashabiki ambao wanatamani nifanye kile nilichokifanya msimu uliopita.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad