Meneja wa Cheed, Killy Kutoa Tamko Kufukuzwa Wasanii wake Konde Gang



Saa chache baada ya uongozi wa lebo ya Konde Music Worldwide kutangaza kusitisha mkataba na wasanii Ally Omar ’Killy’ na Rashid Mganga ’Cheed’ , meneja wao aahidi kutoa tamko baadaye ya leo.
Meneja huyo anayeitwa, Lawi Cosmas ’Lawize’ ameiambia Mwanaspoti kuwa ni mapema kusemachochote kwa sasa kwakuwa taarifa hiyo nao wameiona kwenye mitandao na hawajapatabarua rasmi ya kimaandishi.

“Hata sisi ndugu mwandishi na wasanii wangu hatujui nini kimetokea hadi sasa, naomba unipe muda mpaka tuwasiliane na uongozi tutakuja na tamko letu rasmi kuhusu hatua hii , kwakuwa nasi tumeiona tu huko mitandaoni,” amesema Lawize
Aidha Meneja huyo amebainisha kuwa katika maamuzi hayo hawajashirikishwa kwani hata juzi katika kundi lao la WhatsApp la ofisini walitakiwa kuhudhuria bila kukosa katika sherehe ya kutimiza miaka minne tangu kuanzishwa kwa lebo ya Konde.

Hata hivyo alisema yeye hakwenda na wala hajui kama wasanii wake hao walikwenda au la.
Kwa miaka miwili waliyokuwepo Konde Music,Killy aliweza kutoa nyimbo nne ikiwemo Mwisho, Vumilia , Roho na Ni Wewe wimbo aliomshirikisha Harmonize na ambao ndio wimbo wake uliofanya vizuri kuliko zote tangu atue kwenye lebo hiyo.

Ni Wewe ni wimbo uliotumia midundo ya wimbo wa Sina Makosa uliowahi kuimbwa na bendi ya Les Wanyika wimbo ambao pia uliwahi kurudiwa na Cool James mtoto wa Dandu.
Kwa upande wake Cheed akiwa konde alitoa nyimbo tatu ikiwemo Wandia, Final na Ndoa.

Wakiwa lebo ya Kings ,walishiriki kuimba nyimbo mbalimbali ukiwemo Masozy, Rhumba, Mwambie Sina na Toto walioimba kwa pamoja wasanii wote wa lebo hiyo akiwemo Alikiba ikiwa ndio mara ya kwanza lebo hiyo ilipotambulishwa kwa umma.

Lakini pia Killy aliweza kuepua vibao vingine ikiwemo Gubu aliomshirikisha Alikiba, Chumbani aliouimba na K2GA msanii ambaye mpaka leo yupo kwa Alikiba

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad