Messi athibitisha Qatar ndiyo kombe lake la mwisho la Dunia



Tunaweza kusema kuwa zama za Messi na Cristiano Ronaldo zimefika ukingoni na sasa dunia itaanza kushuhudia damu changa na kizazi kipya cha kina Erling Haaland, Kylian Mbappe na wengine wakijaribu kuzitafuta rekodi za hao wababe wa soka na vipenzi vya mashabiki wa kabumbu ulimwenguni.


Staa wa Argentina, Lionel Messi amethibitisha kuwa Kombe la Dunia nchini Qatar kwake litakuwa ndiyo la mwisho na hapo ndipo tunaposema mwisho wa zama za Ronaldo na Messi zimekaribia.


Mwezi ujao ulimwengu itamshuhudia Messi akiwa kwenye michuano ya kombe la Dunia kwa mara yake ya tano na ya mwisho na kutundika daluga katika mashindano hayo na kuwaachia damu changa kuendelea kulipigania taifa la Argentina.


“Je, ni Kombe langu la mwisho la Dunia? Ndiyo, hakika ndiyo, hakika ndiyo. Nina hesabu siku tu kuelekea Kombe la Dunia,” Messi alipokiambia chombo cha habari cha Star+. “Ninahesabu siku hadi Kombe la Dunia.


Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona Kombe la Dunia Qatar 2022 litakuwa la tano kucheza, katika michezo 164 aliyotumikia timu ya taifa lake amefunga jumla ya magoli 90 tangu alipoanza kuliwakilisha mwaka 2005.


Wengi wangetamani kuwaona Messi na Ronaldo wakiendelea katika michuano hiyo lakini kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad