Mhubiri James Ng'ang'a afichua sababu kwa nini alioa mke mdogo



Mhubiri maarufu James Ng'ang'a wa Neno Evangelism Ministry ametetea hatua yake ya kuoa mke mdogo zaidi.

Wakati akiwahutubia waumini wa kanisa lake katika ibada  ya hivi majuzi, mhubiri huyo mwenye umri wa miaka 69 alibainisha kuwa mtu hujitosa kwenye ndoa na yule amtakaye wala sio yule jamii inamtaka.

Alifichua kuwa alikosolewa vikali na viongozi wa kanisa wakati alipoamua kufunga ndoa na mwanamke mdogo.


"Nikioa huyu wazee wa kanisa walisema 'anaoa mtu mdogo', nikasema 'ni wa kukula? ni wako? ama ni wa kuuza'," alisema.

Aliongeza "Mke si wa Mungu, ni wangu. Iwe ni mdogo ni wangu," 

Ng'ang'a aliweka wazi kwamba hakuwa tayari kuoa mwanamke mzee.

"Nilipiga hesabu nikaona, ningechukua kama hawa wazee alafu tukianza kunywa dawa za pressure, tukunywe wawili siku moja na hatujui. Kisha tuulizane kama tumekunywa, tumeze tena sisi wawili tukutwe huko??" alisema.


"Alafu baridi ikiwepo alafu tuwashe jiko tuweke kwa nyumba tukutwe tumekufa!"

Mtumishi huyo wa Mungu mwenye utata mwingi aliwashauri wanaume kuwabembeleza wapenzi wao kwa maneno matamu na zawadi.

Hata hivyo, aliwaonya dhidi ya kuwaabudu na kuwapigia magoti hasa wakati wanapokosea.

"Sisi huwa hatupigii wanawake magoti, lakini huwa tunawanunulia kakitu tu. Unakuja na kakitu. Yeye ndiye atapiga magoti akwambie pole. Ukitaka mke wako aone umejuta, unamnunulia kitu unakuja nayo," alisema.


Kwa sasa Ng’ang’a yupo kwenye ndoa na Loise Murugi ambaye pia anahudumu kama mtume katika mojawapo ya makanisa yake.

Wanandoa hao wawili walifunga pingu za maisha mwaka wa 2012, lakini maisha yao ya ndoa hayajawa nyororo kila wakati.

Mwaka wa 2015, Loise aliwasilisha ombi la talaka na kumshutumu mhubiri huyo kwa kumshambulia, kuenda nje ya ndoa,  kutowajibika na kunywa pombe.

Hata hivyo, wawili hao walipatanishwa baadaye kufuatia kuingilia kati kwa viongozi wa kanisa.l

Hapo awali, Ng'ang'a aliwahi kufichua kuwa aliyekuwa mkewe wa kwanza ambaye alikuwa amejaliwa mapacha naye aligura ndoa yao baada ya kuacha amemdanganya kuwa ameendea nguo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad