Mkwasa: Yanga ni yule namba 6 tu




KOCHA mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa amesema kupoteza mchezo wao na Yanga ni uzoefu ndio uliowabeba ndani ya dakika 90 za mechi hiyo ya raundi ya tano ya Ligi Kuu Bara.

Ruvu Shooting ilifungwa mabao 2-1 mchezo uliochezwa juzi usiku katika Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mkwasa ambaye ni mchezaji, kocha na kiongozi wa zamani wa Yanga, alisema: “Kiungo wao namba sita (Yanick Bangala) alikuwa huru kusogea lakini viungo wangu walijitahidi kuzuia, mabeki wangu pia walipambana na kumfanya hata yule wa kutetema asiteteme.”

Mkwasa ambaye kikosi chake kipindi cha kwanza kilionekana kucheza kwa kujilinda zaidi mbinu ambayo iliwafanya waende mapumziko wakiwa hawajafungana, lakini kipindi cha pili timu hiyo ilifunguka.


Akizungumzia jambo hilo, Mkwasa alisema aliamua kufunguka baada ya kuruhusu bao na kuona amtoe beki wa kati Tariq Abied na kumuingiza mshambuliaji ili kupeleka kasi.

“Tulilazimika kufanya mabadiliko na alipoingia Chanongo (Haruna) alibadilisha mchezo kwa kiasi kikubwa, muda mwingine mabadiliko kama haya inakuwa bahati nasibu, inawezekana tungemuanzisha tungekuwa na matokeo tofauti zaidi.”

Chanongo alikuwa mwepesi wa kupeleka mashambulizi akitokea upande wa kulia na kumpa tabu beki wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa katika kukabiliana na.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad