Mpenja "Mtu Anapigwa 2-1 Leo"



Nabi yupo kwenye presha kubwa kutokana na malengo ya Yanga yalikuwa kucheza hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika na imeshindikana kuwa hivyo baada ya kuondolewa na Al Hilal ya Sudan.

“Salama ya Nabi au kuondoa presha kwake ni kupata ushindi dhidi ya Simba ili aweze kupiga hesabu nzuri za kwenda kucheza mchezo wa hatua ya mtoano kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Club Africain. Ushindi utarejesha hata furaha kwa mashabiki ambao wamekuwa wakitamba mitaani kwa muda mrefu haswa kabla ya Yanga kuingia kwenye msimu mpya wa kimataifa ambao matokeo yamekuwa tofauti na matarajio yao.

“Presha itaondoka kwa Nabi baada ya kumfunga Mnyama na furaha ndani ya Yanga itarudi na kusahau kama waliondolewa kwenye Ligi ya mabingwa Afrika huo ndio utamaduni wa soka letu lilivyo.”

“Mgunda kwake mambo yapo freshi na amewashika viongozi wa Simba kwenye eneo zuri kwa sasa kutokana na matokeo bora aliyoyapata kwenye mashindano ya CAF pamoja na yale ya ndani.”


“Kama Mgunda atashinda mechi hiyo ya Yanga maana yake atakuwa kipenzi cha mashabiki, ataendelea kuaminiwa na huenda akamaliza msimu akiwa kwenye nafasi hiyo kwani matokeo mazuri yatakuwa yanampa nguvu nyuma yake. Na itasitisha hata azma ya Simba kumtafutia bosi wake.

“Mgunda miongoni mwa eneo muhimu alilofanikiwa ni kuwapa heshima kubwa wachezaji wazoefu na kuishi nao kama watoto wake na kila mmoja kuhisi anaweza kufanya jambo zuri kwenye timu wachezaji hao wote wamepata morali kwa sasa na wanakwenda kufanya kazi.”

“Si ndani ya uwanja tu, hata ukiangalia anavyoishi na kufanya kazi na viongozi wenzake kwenye benchi la ufundi utagundua umoja ni nguvu na Simba wamekuwa kitu kimoja.”


MECHI MBILI ZA DABI

“Mechi mbili kubwa za Simba na Yanga nilizotangaza ni ile ya Machi 8, 2020 ambayo Yanga ilishinda bao 1-0, likifungwa na Morrison kwa faulo kali baada ya Jonas Mkude kumchezea rafu. Mechi hiyo Rais Magufuli alikuwa Uwanjani nakumbuka;

“Ukubwa wa mechi hiyo ilitokana na ujio wa Magufuli na aina ya bao la Morrison hata staili yake ya kushangilia ilikuwa kivutio kwa watu wengi waliofuatilia mchezo wenyewe,”

“Mechi nyingine iliyokuwa kali kwangu kutangaza na aina yake ni ile ya Januari 4, 2020 Simba ikitangulia kwa mabao mawili kabla ya baadae Yanga kuja kusawazisha na waliishika hiyo mechi dakika za mwisho hadi Mnyama alikaa kimya na kuomba mechi iishe.”

MABAO MENGI

“Kutokana na vikosi vyote viwili vilivyo sasa hivi ni ngumu mechi hiyo kumalizika kwa mabao mengi sana. Lakini hakuna suluhu wala sare ya mabao kama 3-3. Naona ushindi wa bao 1-0 au mabao 2-1 na yoyote anaweza kushinda mechi hiyo, matokeo hayo nasema kwa jinsi ninavyoziona timu zilivyojipanga na tabia za dabi zinavyokuwa.”


“Wakati timu hizo zilipokuwa zinazalisha mabao mengi sita na kuendelea kuna moja inakuwa ipo chini kwenye kiwango zaidi ya mwenzake ila ukiangalia kwa wakati huu kama zote mbili hazijaachana mbali na zinalingana.

“Mechi hii naiona inaweza kwenda kuzalisha si zaidi ya mabao matatu inaweza kuwa 1-1 au mmoja akafungwa bao 1-0 au mabao 2-1 sioni matokeo mengine zaidi ya hayo,” anasema Mpenja na kuongeza;

“Naona matokeo hayo kwani mechi ubora wa wachezaji hautofautiani na tutakwenda kushuhudia mpira mkubwa ukichezwa na utakuwa mchezo yenye mbinu nyingi ndani yake na kila mmoja akitumia silaha yake,”

“Simba itakwenda kucheza mpira na kupasiana pasi nyingi kwani huo ndio ubora wao wakati Yanga itakwenda kucheza mipira mirefu kwani ina wachezaji wengi wenye uwezo wa kukimbia haswa wale wa pembeni.”


UTAMU WA TUISILA

“Tuisila Kisinda tangu amerejea kwenye kikosi cha Yanga bado hajaonyesha makali yake haswa watu wengi walivyokuwa wanategemea kama ilivyowahi kuonyesha kabla ya kuondoka nchini. Hivyo wikiendi hii inaweza kuwa habari tofauti kama ataamua. Tuisila miongoni mwa mechi aliyocheza vizuri dhidi ya Simba ni ile ya Novemba 7, 2020 iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1, bao la Yanga lilifungwa na Michael Sarpong.”

“Tuisila alikuwa wa moto alimkimbiza Onyango hadi kusababisha mkwaju wa penalti ambayo Sarpong alifunga kutokana na ukubwa wa mechi hii anaweza akapewa nafasi na akacheza kwa kupania kama ilivyokuwa kwenye mchezo huo.”

“Kama wachezaji wa Simba watamuacha Tuisila akacheza kwa uhuru na kupata nafasi ya kupokea mipira mirefu ile ya kukimbia anaweza kuwadhuru wapinzani wao kutokana na uwezo wake wa kukimbia,”

“Nikiangalia kwenye kikosi cha Simba hakuna beki ambaye anaweza kumfikia Tuisila kwa kikimbia kwa maana hiyo kama atakuwa anapata mipira hiyo mirefu atakwenda kuwapa wapinzani wao wakati mgumu muda wote.

“Augustine Okrah ndio mchezaji anayeweza kumfikia Tuisila kwa mbio sasa hatakuwa na nafasi ya kumkaba kwani muda muda mwingi anakwenda kushambulia na kukaba si kazi yake ya mara kwa mara.”


“Lakini yote kwa yote twendeni Uwanjani tukaangalie mechi kali na yenye ushindani. Itakuwa mechi nzuri sana kuwahi kutokea kwa watani wa jadi tukutane uwanjani. ”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad