Mrembo wa Tanzania Hadija Kanyama Ametwaa Taji la Urembo la Dunia kwa viziwi


Mrembo wa Tanzania Hadija Kanyama ametwaa taji la urembo la dunia kwa viziwi katika shindano lililofanyika Dares Salaam na kutangazwa ushindi huo na jopo la Majaji 8 wakiongozwa na Rais wa Mashindano hayo kutoka nchini Marekani, Mama Baneta Ann Li.


Ukiacha kuwa Miss Dunia na kuwabwaga Washiriki wenzake 12 kutoka Mataifa mbalimbali, Hadija pia ameshinda kipengele cha Miss katika kucheza muziki wa asili, huku kwa upande wa Mr. Kiziwi, ushindi umeenda kwa Gareth Kelaart, kutoka nchini Australia.


Mgeni rasmi katika Fainali hizo za Miss Kiziwi alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Doroth Gwajima akimwakilisha Rais Samia huku Mgeni maalumu akiwa Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mohamed Mchengerwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad