Mtoto Aliyefanyiwa Upasuaji Kutoa Jembe Lililokwama Kichwani Afariki Dunia





Mvulana huyo alikata roho katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) Jumanne, Oktoba 11, akifanyiwa upasuaji wa kuondoa jembe

Awali kulikuwa na ghadhabu kutoka kwa umma baada ya kuibuka kuwa madaktari walikosa kumshughulikia mtoto huyo zaidi ya saa 20 baada ya kufika hospitalini humo akiwa katika hali mahututi.

KNH baadaye ilitoa taarifa kwenye mitandao yake ya kijamii ikieleza ni kwa nini madaktari walichukuwa muda mrefu kumhudumia mtoto huyo ambaye aliripotiwa kuwa katika hali mahututi.


Jamaa Aliyefungwa Kimakosa Aachiliwa Miaka 33 Baadaye; Amwaga Machozi Akisimulia Yaliyomfika
"Mgonjwa alikuwa amepoteza damu nyingi, na kutokana na hali yake, utaratibu wa kuganda haukufanyika kama ilivyotarajiwa, na hivyo kuchelewesha upasuaji kwa sababu ingekuwa hatari kwa mgonjwa," ilisoma sehemu ya taarifa hiyo.

Mama yake malaika huyo, Judy Muthoni, alilaumu hospitali hiyo kwa kuchelewa kumtibu mwanaye ambaye aligongwa na jembe kwa bahati mbaya Jumatatu jioni na kaka yake walipokuwa wakicheza.

Maoni ya Wakenya
Wakenya waliovunjika moyo walijitokeza kwenye mitandao ya kijamii kumuomboleza mvulana huyo huku baadhi wakiwakashifu madaktari kwa kuchelewa.


Judy Maxeen Kwamby alisema: "Hii inanivunja moyo jinsi nilivyokuwa nikimuombea mtoto asiye na hatia anusurike. Tukio lisiloweza kuvumilika zaidi ambalo mama yake atakuwa nalo. Mungu auponye moyo wake."

Kate Catherine Muniu alisema: "Mwenyezi Mungu amfariji mwanamke huyu. Hili ni jambo la kuhuzunisha sana. Kama mama, nilipoteza nguvu. Ni Mungu pekee anayeweza kuwalinda watoto wetu."


Mathew Mogambi alisema: "Ninaomba na natumai kaka yake atakuwa na nguvu za kutosha kukabiliana na hali hii katika siku zake za baadaye maishani. Ni lazima hakika itamletea madhara akijua kwamba alihusika katika kifo cha kaka yake."

Georgina Wambua alisema: "Moyo wangu umevunjika...naweza kufikiria uchungu aliopitia mtoto. Ni mtu hodari,.. saa zote hizo akiwa na jembe kichwani. Naweza kufikiria kile wazazi wanapitia."


Kama ilivyoripotiwa awali, Cyrus Maina alimsaidia mvulana huyo kupata huduma ya kwanza na X-ray katika Hospitali ya Thika Level 5 kabla ya wasamaria wema kulipia ambulensi na kulazwa, kwake KNH.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad