Mtoto anyongwa Kagera, wawili wakamatwa



Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera, linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Aisha Issa (3), ambaye anadaiwa kunyongwa shingo kwa kutumia kamba ya nailoni iliyokutwa kwenye shingo yake, Septemba 29, 2022, mtaa wa Matopeni, Kata ya Kashai, Manispaa ya Bukoba.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Kagera William Mwampaghale, amesema kuwa mtuhumiwa wa kwanza alikamatwa siku ya tukio na kumtaja mtuhumiwa mwingine ambaye alishirikiana naye kufanya mauaji hayo, ambaye pia amekamatwa na jeshi hilo Oktoba 03 mwaka huu

Kufuatia tukio hilo Mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila, alikwenda kuhani msiba katika familia iliyopoteza mtoto huyo, na akiwa katika eneo hilo alisema kuwa jitihada mbalimbali zinafanyika kukomesha vitendo vya mauaji, na kwamba ndiyo maana vinafanyika vikao na watendaji wa vijiji, mitaa, kata na maafisa tarafa, ili kuhakikisha amani ya mkoa inakuwepo.

Siku ya tukio mtoto Aisha alitoweka nyumbani kwao na baadae baada ya msako kuanza mwili wake ulikutwa katika nyumba ambayo haijaisha iliyoko katika mtaa wa Matopeni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad