Mtoto wa 50 CENT Ataka Kumlipa Baba yake Kiasi Cha Child Support Anayopewa Kusudi Apate Walau Masaa 24 ya Kukaa Naye


Mtoto mkubwa wa rapa 50 Cent, Marquise Jackson (25) ameonyesha wazi kuwa anacho miss kutoka kwa baba yake ni muda wa baba yake na wala sio Child Support anayo pewa kila mwezi. Hivi karibuni Marquise alifanya interview na kudai kiasi cha Dollar za kimarekani 6,700 zaidi ya milioni 15.6M za kitanzania anacho pata kwa baba yake kila mwezi kama Child support hakitoshi, ni anakatiliwa kwa baba ambaye anajiweka wazi kuwa ana beef na kila mtu, ana matatizo na kila mtu, kama mtoto hawezi ishi sehemu yoyote ile kwa usalama wake, hivyo ni kiasi kidogo kutafuta usalama wake.

Ikiwa ni siku chache tu baada ya interview hiyo, Marquise ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa, “wote mnapo fikiria kuwa dollar 6700 ni pesa kubwa, mtu mmoja amwambie baba yangu kuwa nitamlipa kiasi hicho kwa masaa 24 pekee ya muda wake, hivyo tunaweza fanya kila kitu ambacho nilitamani kufanya naye kama mtoto”

Kauli ambayo imeonyesha kijana anamiss mapenzi ya baba yake na sio pesa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad